Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo na Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu (CSC) chenye makao yake Mkoani Arusha, Colonel Verus Chrysostom Mbuzi katika ziara maalumu ya kimafunzo iliyofanywa na Maafisa hao wa ngazi za juu wa Kijeshi kutoka mataifa mbalimbali katika Kampuni ya Mati Super Brands Ltd.
Mulokozi amesema kuwa Tuzo hiyo inawapa chachu ya kuendelea kufanya vizuri kuendelea kushirikiana na taasisi za umma Pamoja na kuzalisha bidhaa bora zinazozingatia ubora na usalama wa mtumiaji.
Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu (CSC), Colonel Verus Chrysostom Mbuzi amepongeza Kiwanda kwa kuwa karibu na jamii na taasisi za Serikali pamoja na kutoa fursa wa mafunzo kwa vitendo vya Maafisa wa Kijeshi juu ya masuala mbalimbali ikiwemo usalama wa chakula.