Jesusie
JF-Expert Member
- Aug 29, 2021
- 1,466
- 766
===
Chuo Cha Usimamizi wa Fedha na Biashara CBE nchi Tanzania kimemtunuku Mhe David Zacharia Kafulila ngao ya heshima kwa uchapakazi wake uliotukuka kwa Taifa lake la Tanzania.
Mkuu wa chuo hicho Prof. Eddnah Luoga amesema chuo chake kimeamua kumtunuku ngao hiyo ya heshima katika kutambua juhudi zake kwenye kumpata mbia mwekezaji toka sekta binafsi atakayejenga mabweni katika chuo hicho yatakayokuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi elfu 12 kwa mara moja au kwa Mkupuo.
Mwekezaji huyo atawekeza kwa sharti la Ubia ili kukabiliana na changamoto za wanafunzi kuishi mbali na eneo la chuo hicho jambo ambalo hupunguza zaidi ari, ufaulu na nguvu za kimasomo kwa wanafunzi wa chuo hicho hasa wanaoishi mbali na mazingira ya chuo hicho.
David Zacharia Kafulila Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Ubia kati ya Serikali na Sekta binafsi Tanzania PPPC amekuwa akisisitiza wakati wote kuwa lazima Tanzània ifike wakati ambao Serikali yetu itapunguziwa mzigo katika kutekeleza miradi yake ya maendeleo hasa ile yenye sura ya kibiashara.
Mkurugenzi huyo anasema kwa kufanya hivyo kutaipunguzia Serikali hiyo mzigo na kuifanya itekeleze baadhi ya miradi yake ya maendeleo nje ya bajeti yake hasa ile yenye sura ya kibiashara kama huu wa Ujenzi wa mabweni ( projects contraction outside the government balance sheet )
===