Chuo Kikuu cha Biashara (CBE) chamtunuku David Kafulila ngao ya heshima kwa kusimamia ukuzwaji wa sera za Uchumi Jumuishi nchini

Jesusie

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2021
Posts
1,466
Reaction score
766

===
Chuo Cha Usimamizi wa Fedha na Biashara CBE nchi Tanzania kimemtunuku Mhe David Zacharia Kafulila ngao ya heshima kwa uchapakazi wake uliotukuka kwa Taifa lake la Tanzania.

Mkuu wa chuo hicho Prof. Eddnah Luoga amesema chuo chake kimeamua kumtunuku ngao hiyo ya heshima katika kutambua juhudi zake kwenye kumpata mbia mwekezaji toka sekta binafsi atakayejenga mabweni katika chuo hicho yatakayokuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi elfu 12 kwa mara moja au kwa Mkupuo.

Mwekezaji huyo atawekeza kwa sharti la Ubia ili kukabiliana na changamoto za wanafunzi kuishi mbali na eneo la chuo hicho jambo ambalo hupunguza zaidi ari, ufaulu na nguvu za kimasomo kwa wanafunzi wa chuo hicho hasa wanaoishi mbali na mazingira ya chuo hicho.

David Zacharia Kafulila Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Ubia kati ya Serikali na Sekta binafsi Tanzania PPPC amekuwa akisisitiza wakati wote kuwa lazima TanzΓ nia ifike wakati ambao Serikali yetu itapunguziwa mzigo katika kutekeleza miradi yake ya maendeleo hasa ile yenye sura ya kibiashara.

Mkurugenzi huyo anasema kwa kufanya hivyo kutaipunguzia Serikali hiyo mzigo na kuifanya itekeleze baadhi ya miradi yake ya maendeleo nje ya bajeti yake hasa ile yenye sura ya kibiashara kama huu wa Ujenzi wa mabweni ( projects contraction outside the government balance sheet )
===


 
Bweni la wanafunzi 12?
Hilo ndio limemfanya atunikiwe??
 
View attachment 3101793

Chuo kikuu Cha Usimamizi wa Fedha na Biashara Cha CBE nchi Tanzania kimemtunuku Mhe David Kafulila ngao ya heshima kwa uchapakazi wake uliotukuka.​
Vyuo huwa vinatoa digrii za heshima hayo ya ngao Chuo kutoa ndio nayasikia leo

Ngao mara nyingi hutolewa na machifu kwa mhusika

CBE wameanza kutoa ngao kama chuo?
 
Mbona ghafla hivyo?
 
Vyuo huwa vinatoa digrii za heshima hayo ya ngao Chuo kutoa ndio nayasikia leo

Ngao mara nyingi hutolewa na machifu kwa mhusika

CBE wameanza kutoa ngao kama chuo?
Huu wako ni uzoefu au ndio practice?
 
Nashangaa hata mimi hivyo ni sawa na vyumba vitatu vyenye double deck mbili za wanafunzi wanne kila chumba
Hayo ndio mafanikio ya PPP hadi apewe tuzo hiyo?
appreciation ni jambo jema,

Hebu angalia wanafunzi elfu 12 watapata mabweni,

Nauli hazitawahusu tena kila siku,

Mimi nadhani Kafulila deserves more than that,
 
Siasa tu hizo.
 
appreciation ni jambo jema,

Hebu angalia wanafunzi elfu 12 watapata mabweni,

Nauli hazitawahusu tena kila siku,

Mimi nadhani Kafulila deserves more than that,
Tatizo lako Ume edit uliandika 12 huna hata haya kukiri kuwa ulikosea kuandika badala ya 12 ni elfu 12
Unaandika makosa unarekebisha kimya kimya

Anyway all in all tusubiri yajengwe ndio nitapongeza

Binafsi simuoni mtu ni mchapa kazi hadi nione matokeo mambo ya tuko mbioni,tunatarajia ,tuna mkakati sio muumini wa empty words kama hizo kuwa nipige makofi au kutoa tuzo
 
Ngoja tuone ila nadhani mpaka wanatoa tamka kila kitu kitakuwa sawa
 
Kafulila anaakili sana huyu jamaa ila hako kanafasi hakana impact sana
 
Kafulila asisitize Serikali iuze Shirika la ndege (ATCL), asisitize wawekezaji binafsi katika umeme kuondoa monopoly ya TANESCO
ChoiceVariable
Hata TTCL ni majanga sana, haya ndiyo maeneo ayatupie macho sasa ili kuleta ufanisi na tija
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…