Wamba de Wamba
Member
- Sep 2, 2013
- 16
- 2
Ni muda sasa tokea Chuo hiki kianze ambacho kimekuwa kikimwagiwa sifa kipindi kikianza. Nilianza kusikia sifa hizo nyingi na kupata hamu ya kusoma katika chuo hiki lakini haikuwa bahati yangu na Mola akanipeleka Makerere. Cha kushangaza sifa hizi nilizokuwa nikizisikia zillianza kuporomoka na mabaya kushika kasi. Niliyasikia mazuri na sasa mabaya ambayo naamini kila mtanzania anayasikia. Kwa upande wangu niliyasikia na ninayasikia lakini si kwakuyapuuza kivile.
Lakini imefika mahala haya mabaya sasa yamezidi kiasi kwamba kila kona ya mitandao yanatajwa. Leo hii napenda kusema kuwa inaonesha ni kweli haya yanayosemwa. Tatizo hapa ni utawala wa Chuo ambao sasa kila kona unalalamikiwa. Baba wa Taifa, Mwl. Nyerere aliweza kuzuia matabaka katika Taifa letu na viongozi wanaoendekeza hili si mbaya kuwaona kuwa wana ombwe la uongozi. Kwa kudhibitisha, leo nilitembelea website ya chuo nikakuta tangazo juu ya skolaship za somo la hisabati kwa kushirikiana na chuo cha albata. Ukisoma vizuri tangazo hili utaona sehemu za mwisho linatugawa kwa kuweka misisitizo isiyo na tija. Mbona twafanya haya na isitoshe ni hivi majuzi hata Rais wetu alikataa haya yalipotaka kujitokeza ya Mtwara. Ebu msitake kutugawa Watanzania, sisi ni wamoja. Mungu ibariki Tanzania,