Chuo kikuu cha ekernforde hakijasajiliwa na baraza la famasi kutoa mafunzo

Chuo kikuu cha ekernforde hakijasajiliwa na baraza la famasi kutoa mafunzo

assuredly4

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2011
Posts
1,216
Reaction score
220
Nimepata taarifa kuwa Chuo kikuu cha Ekernforde kilichopo Tanga hakijasajiliwa na Baraza la Famasi kutoa mafunzo ya ngazi ya cheti (Certificate in Pharmaceutical Sciences) na diploma (Diploma in Pharmaceutical Sciences). source Mwananchi Novemba 14, 2012 uk.12 . nimetype ili kuwafikishia gt taarifa sahihi

JAMHURI YA MUUNGANO TANZANIA
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
BARAZA LA FAMASI


TAARIFA KWA UMMA

KUHUSU CHUO KIKUU CHA EKERNFORDE KUDAHILI WANAFUNZI WA CHETI (CERTIFICATE) NA STASHAHADA ( DIPLOMA IN PHARMACEUTICAL SCIENCES) KWA MWAKA 2012/2013
Baraza la Famasi linapenda kutoa ufafanuzi kwa umma kuhusu Tangazo la Chuo Kikuu Cha Ekernforde - Tanga kuanza udahili (admission) wa wanafunzi katika ngazi ya cheti na diploma katika pharmaceutical sciences, katika gazeti la Mwananchi la tarehe 10 Oktoba 2012 toleo ISSN 0856-7573 Na. 04490. Baraza la Famasi ni Taasisi ya Serikali iliyoko chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii iliyoanzishwa chini yaSheria ya Famasi Na. 1 ya 2011. Baraza hili pamoja na majukumu mengine limepewa wajibu wa:- 1. kuhakiki na kupitisha (approval) Mafunzo na Mitaala inayohusu taaluma ya famasi nchini kwa mujibu wa vifungu 4(i),(p) na 5(h)2. Kuhakiki, Kusajili na kupitisha Taasisi za Elimu na Mafunzo ya Taaluma za Famasi nchini, na3. kusajili wataalamu wa taaluma ya famasi nchini . Kwa kuzingatia Sheria ya Famasi, 2011, Baraza linapenda kutoa taarifa kwa umma kuwa Chuo Kikuu Cha Ekernforde kilichopo Tanga Mjini hakijaidhinishwa wala kusajiliwa na Baraza na hivyo hakitambuliwi wala hakikubaliki na Baraza kutoa mafunzo ya aina yo yote ile katika taaluma ya dawa (certificate, diploma or bachelor in pharmaceutical sciences). Vilevile hata mitaala yake ya kufundishia haijaidhinishwa wala kusajiliwa wa Baraza. Kwa Taarifa hii, Baraza linawatahadharisha wananchi kutotumia chuo hiki kutokana na ukweli kuwa hakitambuliwi kisheria na Baraza la Famasi kwa vile hakijawasilisha taarifa wala kusajiliwa na Baraza. Taasisi yoyote inayokusudia kutoa mafunzo ya dawa, ni lazima ipate idhini ya Baraza ili wanafunzi waweze kusajiliwa pindi watakapokamilisha mafunzo yao. Baraza linasisitiza kuwa kutokana na Chuo hiki kutokidhi masharti na vigezo vya Sheria, wanafunzi watakaosoma katika Chuo hiki hawatatambuliwa wala kusajiliwa na Baraza hivyo kupoteza sifa ya kuajiriwa Serikalini, Taasisi binafsi, na hata kujiajiri. Baraza linapenda kuwasisitizia wananchi ya kuwa kabla ya kumwandikisha mtoto wako katika chuo chochote kinachoendesha masomo ya fani ya famasi, ni muhimu mwenye chuo akuoneshe kibali cha Baraza. Imetolewa na: Msajili, Baraza la Famasi, S. L. P. 31818, Dar es Salaam.Kwa mawasiliano, Simu: 022–2451007 au 0684/0755-881677/0655881676
 
hili baraza lilikuwa wapi mpaka chuo kinafanya udahili na wanafunzi wanaanza masomo?
wao kama baraza la famasia walipaswa kutoa taarifa mapema na ingewezekana kuzuia udahili kabisa mpaka watakapokamilisha vigezo vyao!
 
Sasa hilo baraza limechukua hatua gani za kisheria dhidi ya hicho chuo kwa Mfano kukifungia, kukipiga faini, kukiamuru kulipa fidia au kukishitaki?

Au ndio mambo kama yale yale ya Mkwele kubaki kulalamika tu wakati mamlaka anayo.

What will happen if the college will continue to conduct those studies although it has been warned?
 
Yale yale ya kuwaambia mafisadi warudishe hela alizofisadi. Hii ndio Tanzania....
 
Kama kawaida yangu nasema na anayetaka kunukuu anukuu "HAKUNA WIZARA YENYE UMUHIMU KWA WATANZANIA ILA YENYE MAMBO YA KIPUMBAVU KAMA SI YA KIS******** KAMA WIZARA YA ELIMU" sijui hii nchi inaenda wapi toka enzi za akina Kapuya, Mungai, Maghembe, Kawambwa nk wote hawa wametoa maamuzi ya kipumbavu ambayo hata kichaa asiye na akili hawezi kufanya
  • kuunganisha masomo
  • kufuta masomo
  • kufuta michezo
  • kubadili mitaala (sylabus) mara kwa mara bila sababu
  • kufuta mitihani yenye tija katika kuchuja uwezo wa wanafunzi
  • kupunguza muda wa masomo kwa wahitimu wakidhani wanaboresha kumbe wanawaumiza wadogo zetu bure
  • kukubali form 1 wasiojua kusoma na kuandika kuendelea na masomo eti wanamaintain enrollment status
  • shule za kata ha ha ha ha ha ha ha ha hapo sasa (hakuna walimu japo walimu wanatoka vyuoni kila mwaka, madarasa hayatoshi, madawati pia bado vitabu na nyenzo nyingine za kufundishia, maabara hakuna, maktaba hakuna ila hata zingekuwepo kupata vitabu issue nk nk kwa hilo lililotajwa hapo juu wala sishangai system ya elimu ya nchi hii IMEOZA TOTALLY.
 
Hicho chuo kwanza ungekiona, Mungu mkubwa hakina hadhi ya kuitwa Chuo Kikuu sijui watu wanatoa vipi vibali kwa watu kuanzisha such things yani Rushwa zinaipeleka nchi pabaya sana, inauma sana kwa kweli wataalam wanaopatikana katika educational institutions kama hizi wasio na sifa
 
Back
Top Bottom