Chuo kikuu cha katavi kuanzishwa, cha Butiama kiko wapi?

Chuo kikuu cha katavi kuanzishwa, cha Butiama kiko wapi?

tatanyengo

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2011
Posts
1,133
Reaction score
280
Rais Kikwete aliwahi kutangaza kuanzishwa chuo kikuu cha Kilimo huko Butiama kwa kumuenzi marehemu baba wa taifa. Lakini hadi leo hakuna kinachoendelea kuhusu chuo hicho. Gazeti la Majira la leo limeripoti kuwa chuo cha kilimo kingine kitajengwa katika mkoa mpya wa Katavi. Serikali isitoe ahadi zisizotekelezeka.
 
Mmmh hongera kwa serikali kwa hilo lakini ilikuwepo kwenye ilani au ni kwa interest za baadhi tu ya viongozi?Mi nadhani imefika wakati serikali ijenge chuo kikuu kila kanda then kila mkoa si kila kiongozi akiamua na kutaka umma unatangaziwa tu!NYERERE ANGEFANYA HIVYO MUSOMA SI INGEKUWA KAMA ULAYA?

JAMANI SERIKALI MNAVYUO VINGI SANA,VINGI VIKIWA TAABANI !ni kweli tuna upungufu?
 
Huyu ni uchezeaji wa rasilimali tu. Tuna chuo kikuu cha kilimo cha SUA na kuna kingene nimesikia kinajengwa Musoma au Butiama. Kuna vyuo vingine vingi tu vinatoa diploma na cerificates nyingine za kilimo hapa nchini kama Uyole,Tumbi Tabora n.k sidhani kama tunahitaji tena chuo kikuu kingine cha kilimo kwa sasa au hata kwa miongo mitano ijayo. Kwa sasa tunahitaji vyuo vya Science na teknolojia kama MIST AU DIT AU COET. Tatizo la kilimo kwa sasa siyo wasomi ni mbinu na mikakati ya ku-mechanise hiki kilimo chetu kwani kwa sasa kipo too manually.
 
Rais Kikwete aliwahi kutangaza kuanzishwa chuo kikuu cha Kilimo huko Butiama kwa kumuenzi marehemu baba wa taifa. Lakini hadi leo hakuna kinachoendelea kuhusu chuo hicho. Gazeti la Majira la leo limeripoti kuwa chuo cha kilimo kingine kitajengwa katika mkoa mpya wa Katavi. Serikali isitoe ahadi zisizotekelezeka.

Ahadi nyingi za serikali zinatelekelezeka, kinachokosekana ni UTASHI WA KISIASA na upungufu wa hali ya juu kutika kuweka PRIORITIES
 
Back
Top Bottom