KERO Chuo kikuu cha St John's Dodoma hakijapeleka matokeo yetu NACTIVET na kutukosesha fursa ya kuendelea na masomo ya juu

KERO Chuo kikuu cha St John's Dodoma hakijapeleka matokeo yetu NACTIVET na kutukosesha fursa ya kuendelea na masomo ya juu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Nimemaliza chuo kikuu cha st John's Dodoma (st.John’s university of Tanzania ) intake ya 2014/2017 fani ya maabara kwa ngazi ya stashahada(diploma in Medical laboratory ).

Licha ya kuwa nimepata vyeti vyote na kubahatika kusajiliwa na bodi zote zinazohusika na afya na pia hadi sasa nimebahatika kuajiriwa na taasisi za serikali na binafsi.

Changamoto yangu ni kuwa kwa miaka yote hiyo chuo hakijapeleka matokeo yetu NACTIVET hivyo tunashindwa kwenye maombi kwa wale tunaotaka kuendelea na masomo ya juu zaidi kwa kukosa award verification namba (AVN).

Tumejaribu kufuatilia kwa muda mrefu bila mafanikio yoyote chuoni na NACTIVET.

Tunaomba msaada.
 

Attachments

Back
Top Bottom