Sumba-Wanga
JF-Expert Member
- Feb 2, 2011
- 5,353
- 1,234
Nimekuwa najiuliza kama Chuo Kikuu Huria au OUT ni chuo cha serikali. Inakuwaje chuo cha serikali kikawa na mambo ya ajabu namna hii?
Sisi Walimu kutoka nje tuliofanya kazi kama external examiners kwenye kazi za wanafunzi tuna zaidi ya miezi 6 hatujalipwa. Tukiuliza tunaambiwa utaratibu mpya wa Muse unachelewesha malipo. Jambo la ajabu, vyuo vingine vya serikali, kama UDSM na SUA vinavyotumia mfumo huo wa Muse, external examiners wanalipwa.
Haijaishia hapo. Hata wafanyakazi wa OUT hawajapata stahiki zao mbali mbali,.kisingizio kikubwa ni mfumo wa Muse. Hii Muse ya OUT ni tofauti na nyingine?
Swali la kujiuliza, viongozi wa OUT hawalioni hili? Jibu ni rahisi tu, wao wanapata pesa za kusafiri kila wanapotaka, tena ni misululu ya wapambe. Kwa jinsi, hawana haka ya kuhangaikia mfumo ufanye kazi. Everybody for himself, God for us all.
Mwenye macho haambiwi Tazama!
Mungu ibariki Muse,
Mungu bariki viongozi wa OUT
Mungu ibariki Tanzania.