Uwezekano huo upo, niliwahi kusikia kuna mtu mmoja pale utawala, Kitivo cha Sheria, alikuwa anapokea hongo na anambadilishia mtoa hongo matokeo. Yule jamaa nasikia alikuja kuondolewa pale utawala, kitivo cha Sheria. Inawezekana na vitivo vingine mchezo huo umekuwepo vile vile! Hii elimu ya TZ imeoza kila mahali kuanzia Shule za Msingi hadi vyuo kwa wizi wa mitihani, ufundishaji mbovu, kufoji vyeti, nk. Sasa sijui matengenezo yaanzie wapi ndugu yangu!