Naomben msaada juu ya utofaut wa open university na hv vyuo vikuu vya kawaida! afu naombeni kwa anaevifahamu hv vyuo vikuu huria anitajie.nawasilisha hoja!
Chuo kikuu Huria, ni chuo kinachotoa elimu kwa njia ya masafa (distance learning) ambapo mwanafunzi huna ulazima wa kukaa na mwalimu isipokuwa unapewa miongozo ya usomaji na material na unakwenda kujisomea mwenyewe . Utaweza kuonana na mwalimu katika kipindi maalum na pia ukiwa na shida unaweza kumtafuta
Elimu ya masafa ni njia kongwe hapa nchini coz wazazi wetu waliwahi kusoma elimu kwa njia ya redio (rejea mafunzo ya walimu wa UPE enzi za RTDg) na waliweza kumaliza na kufanya kazi vyema kabisa.
Back to the topic: OUT mi nasema ni kichanga coZ ndo kwanza kina miaka 22 sasa tangu kianzishwe, hakina tofauti na vyuo vikuu vingine Tanzania hii isipokuwa utofauti ni katika njia za utoaji wa elimu yake yaani distance vs conventional. Kutokana na uchanga huu na uelewa watu juu ya elimu ya masafa imekuwa ni changamoto nchini mana kuna watu hawataki hata kuisikia wakiamini ni elimu mbaya, ni ya watu wazima, ya waliofeli, hutapata kazi na vitu vingi kibao!!
Mimi binafsi naikubali sana hii shule kwa sababu, inakujenga na self discipline tangu mwanzo!! Wanaoshindwa kujicontrol ndiyo wanaiona hii elimu ngumu na kuiponda bila reason ya msingi.
Inakufanya usiwe tegemezi kwa kujitegemea kwa kila kitu.
Inakufanya uendelee na shughuli zako huku shule inasonga!! Hapo huwezi kuloose mahali.
Nchi nyingi zina vyuo vinavyotoa elimu kwa masafa kwa mfano Open ya Nigeria, India, Zimbabwe, South Africa na n.k. Open zilizofanikiwa zaidi ni za Nigeria na India, watu wao wanazitumia ipasavyo na zimesaidia kuweka wasomi wengi nchini mwao.
La kujivunia kwa OUT yetu ni kwamba mwaka huu pekee imepata tuzo za kimataifa zipatazo tatu mpaka sasa!! Kweli nabii hakubaliki kwao, Watanzania wenyewe tunaiponda kama nini lakini nje wanaikubali sana na ushahidi ni wanafunzi wa kimataifa waliopo! Mwaka jana wamegraduate zaidi ya 20 kutoka Libya na Kenya
Kwa maelezo zaidi nenda vituo vya OUT viko kila mkoa nchini wao watakupa elimu zaidi mie nimewasemea ninapojua ili kukufungua niliponapo tu