A
Anonymous
Guest
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) ni moja kati ya Taasisi za Serikali ambayo hawajali kabisa suala la kulipa pesa za kujikimu kwa Wafanyakazi wao wanaposafiri.
Utakuta mtu anapangiwa kituo cha kazi Simiyu au Katavi na anapaswa kuripoti na ana familia, sio rahisi kuhama na kila kitu let say unatoka Arusha umepangiwa Katavi, hivyo mtu inabidi akaanze upya kwa sehemu kubwa.
Sasa mtu anatazamia hela za kujikimu ili angalau ajipange upya, sadly hizo pesa zinaweza kuchukua hadi mwaka ama zaidi.
Wakati huohuo, haturuhusiwi kukopa kwenye mfumo angalau kuweka mazingira sawa, mfumo unatuhitaji mpaka confirmation. Sasa hii inafanya wafanyakazi wenu wanakuwa watu wa kutembeza bakuli tu na madeni mengi, mnatufedhehesha, tulipeni pesa zetu.
HR Department kwakweli mnatuumiza sana, tuwekeeni pesa na sisi tujione Wafanyakazi kama nyie jamani, au mnataka kutuzima kama batch zingine mlivyowazima.
Pia soma:
~ Madai ya Chuo Kikuu Huria (OUT) kutolipa Watumishi stahiki zao, Chuo chatoa ufafanuzi
~ Uongozi wa Chuo Kikuu Huria wasema utaboresha mazingira ya Kampasi ya Singida
~ Chuo Kikuu Huria - Singida kiboreshe mazingira yake, ni kama vile kimetelekezwa