Makamu Mkuu wa chuo Kikuu Muhimbili amefuta chama cha wanafunzi (MUHASSO), students' Organization kwa kutumia hoja zisizo na mashiko, akidai ni maamuzi ya kikao cha Baraza la chuo cha tarehe 3 Juni 2011 ambacho hakuna uwakilishi wa wanafunzi baada ya kufukuzwa kwa kushinikiza umoja huo kukubaliana na mwongozo wa serikali GN 178 wa 12 juni 2009 uliosainiwa na aliyekuwa waziri wa elimu Prof. Jumanne Maghembe. Kimsingi ni mwongozo kandamizi na haukuwashirikisha wanafunzi wa vyuo.<br><br>lakini cha kushangaza TAHILISO imeduwaa tu. Hii nchi tutafika kweli?