DOKEZO Chuo Kuu Huria hakitoi kwa wakati matokeo ya Mitihani, tunalazimika kutoa pesa kujisajili upya bila kufahamu matokeo

DOKEZO Chuo Kuu Huria hakitoi kwa wakati matokeo ya Mitihani, tunalazimika kutoa pesa kujisajili upya bila kufahamu matokeo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
276
Reaction score
473
Mimi ni Mwanafunzi ninayeendelea na masomo katika Chuo Kuu Huria cha Tanzania (OUT) maarufu kwa jina la Open University ambacho makao makuu yake yapo Kinondoni Dar es Salaam ni kwa muda sasa Wanafunzi wengi katika maeneo mbalimbali nchini tumekuwa tukikutana na changamoto ambayo inatuweka kwenye kizungumkuti.

Tatizo ambalo limeendelea kuwa sugu ni Chuo chetu kutotoa matokeo kwa wakati, mnaweza kufanya mitihani mkiwa 20 wakaleta matokeo ya Watu wawili tu, wengine hawawekewi matokeo na hawatoi maelezo yoyote ya sababu za kutofanya hivyo.

Ikitokea unataka kufuatilia, hakuna kitengo maalumu ambacho kinatoa msaada wa maelezo ya kueleweka kuhusu suala hilo, tunakutana na danadana zisizoeleweka, tunaambiwa wenye changamoto waripoti kwenye vituo vyao, tukifanya hivyo tunaishia kuambiwa changamoto zimetumwa kwenye Kituo Kuu Kinondoni zinafanyiwa kazi, hayo yamekuwa majibu endelevu.

Unaweza kukaa zaidi ya miezi mitano au sita bila matokeo kuingizwa, jambo hilo linatuweka wengi kwenye hali ambayo naiita kizungumkuti kwa kuwa hata kama una mpango wa kuhitimu unashindwa kuelewa upo upande upi, kuna wengine wanalazimika kufanya upya usajili wa mitihani ili waanze kuifanya upya kutokana na kutopatiwa matokeo kwenye mitihani hiyo hiyo waliyofanya awali.

Jambo hilo ni usumbufu mkubwa na limefumbiwa macho wameliacha kama sehemu ya kuvuna pesa maana wanajua wengi wasipoona matokeo wanajisajili upya kufanya mitihani na ukifanya hivyo lazima pesa zikutoke tena.

Kwa mtindo huu wanaoguswa ni wengi na linaendelea bila wahusika kulitatua wala hawaoneshi jitihada za wazi katika kulipatia suluhu wala kutupa ufafanuzi unaoeleweka.

Naomba kutoa wito kwa Wizara ya Elimu itusaidie kupata ufumbuzi wa changamoto hiyo kwa sababu tunapata usumbufu mkubwa ambao unaweza kuepukwa kwa baadhi Watumishi kutimiza wajibu wao, tutazingatia Chuo Kuu Huria ni ofisi kubwa ambayo haitegemewi kuwa na changamoto ya aina hiyo.

Majibu ya Chuo ~ Chuo Kikuu Huria: Matokeo yanatarajiwa kuanza kutoka muda wowote kuanzia leo Januari 27, 2025

Pia soma:
~
Uongozi wa Chuo Kikuu Huria wasema utaboresha mazingira ya Kampasi ya Singida
~ Chuo Kikuu Huria - Singida kiboreshe mazingira yake, ni kama vile kimetelekezwa
~ Chuo Kikuu Huria Tanzania lipeni Waajiriwa wenu pesa zao za kujikimu, mtawaua njaa na kuwafedhehesha mtaani
~ Madai ya Chuo Kikuu Huria (OUT) kutolipa Watumishi stahiki zao, Chuo chatoa ufafanuzi
 
Wahusika watakuwa wamesikia wafuatilie hao walim wanaochelewesha matokeo.
 
Back
Top Bottom