Sema madhara. Sio mazara mangi. Hazina[/QUOTE]
Jamani kama tukiwa practical mtaona kuwa mnayosema 'sio kweli'! Chuchu za chupa za kunyonyeshea SI SALAMA KABISAA na wala hazishauriwi hata siku moja!
Kwa experience yangu....watoto wengi ambao wanapata matatizo ya kuharisha au wanakufa kwa kuharisha (mind you, kuharisha kunachangia karibu 20% ya vifo vya watoto...hii ni serious!) hasa mijini ni kwa sababu ya chuchu/chupa za kunyonyea.
Kiukweli, usafi ndio tatizo la msingi...watu wengi sana hata wenye 'autoclave' machine nyumbani tafiti zimeonyesha kuwa kuna bacteria isolates kwenye chupa na chuchu za kunyonyeshea! Chupa/chuchu zina pindo/corners ambazo ni vigumu kuzifikia wakati wa kuosha especially kama hauko makini, Ukiongezea na tatizo la kuwaacha 'housegirls' kuwa ndio incharge wa huo usafi wenyewe (si katika kuchemsha tuu, hata wakati wa kuandaa na kumpa mtoto maziwa kutumia chuchu/chupa).
Kikombe/bakuli na kijiko ndio njia inayoshauriwa na salama zaidi kuliko chupa. Tatizo mambo ya status ndio yanatuponza tunahatarisha maisha ya watoto wetu. Kunyonyesha kwa chupa kwa akina mama wanaofanya kazi kisha kukamua maziwa asubuhi ni practice ya kawaida sana siku hizi, lakini vile vile ni practice ya hatari sana!