Chupa mpya, mvinyo ule ule...(?)


Mwj1 mnh...fonts zangu hizo Mpenzi...umenishtua!
Au ni uchokozi tu? LOL...

Lol kumbe nimedesa mpaka mwandiko?? Loh...........sijui bwana mambo ya IT mie naonaga maua tu.......... pole kama nimekukwaza.

Naomba kukuuliza...............umesema wewe tabia yako mbaya ni kuwa mbishi loh... huwa unabisha with hoja na kukubali kama umezidiwa au unabisha tu na kwa kuwa wewe ni mwanaume (sorry I respect that) unategemea ukubaliwe na kupewa ushindi??

Weakness yangu nyingine ni kupenda kuliko kiasi....yaani ninajitahidi kuibadilisha hii

Nikipenda huwia inajitahidi kujifitisha kwenye maisha ya mwenzi wangu...........nachange kabisa tabia zangu ili kufit kwenye matakwa yake.....I hate that and am struggling to change>.................
 

bibi na babu hawajakosana wanastahili haki zao halafu ugomvi uendelee kati ya bibie na babuu!!..tutadoo vizuri na nitafurahi vizuri ila asidhani yameisha, nitamkumbushia baadae kuwa ulikosea vile na vile..kwahiyo jirekebishe!!..ila bibi sibanii, tena kwa raha zake anamhitaji babu!!..
 
Dah, Mbu mbona unanitisha hivi, hivi kinyume cha ubishi ni nini? Halafu sasa mbona hata mi mwenyewe sijui kwa nn ni mbishi? Dah au ni kiburi? Au ni kujikweza? Au ni hasira wajameni. Nisaidieni binti mimi, au maneno mengi? Dah au napenda sana sifa? Manake nkipatia nachobisha nafurahi kweli kweli. Dah siwezagi kunyamaza mtu akinisema sema jamani. Uwiii nyie huwa mnafanya je?
 

...ooohh, pole BJ,

Ukiangalia mtiririko wangu hata kwa wengine nao nimegusia zile
-ve traits zao tu.
Kwenye Human Resource Management, hata kama unayemchambua ni housegirl wako,
kuna kitu kinaitwa Personal hidden truths...

Lengo, nia na madhumuni yangu kwa thread hii ni kubadilishana mawazo kwenye 'my hidden self'
na jinsi ya kujiboresha, 'growth!'....Samahani kama nimekukwaza, we'll come back to that.


 

Nimependa kwenye RED hapo


Hapo kwenye BLUE ?:redfaces:

Nilikuwa nimependezwa na comments za huyu mchangiaji...Nadhani sijachakachua thread

 
Reactions: Mbu
Kaka mpendwa nisaidie, nisiwe mbishi basi. Sasa umependezwa na nini? Kutokuwa na mwenza au unashangaa ubishi wangu tu?
 
Kaka mpendwa nisaidie, nisiwe mbishi basi. Sasa umependezwa na nini? Kutokuwa na mwenza au unashangaa ubishi wangu tu?
hayo majukumu unayaweza wewe binafsi na Mungu wako..ila ukishajigundua ndo uhuru wako unapoanzia...Unaposema mwenza unamaanisha nini?..kama ni mume, basi hauko peke yako.

Mleta thread amefanya vizuri, angalau watu wanapata nafasi ya kujichunguza nafisi zao.. Mbu big up
 
Reactions: Mbu

...sasa mwenzio atajuaje umeridhia au hujaridhia bana? Una ishara kama traffic lights? hebu kuwa mpole naweeee...Gubu hilo, lol!!!



Oooppsss, ...Mwj1 mimi hupendelea tu mwisho wa siku points zangu nazo ziwe zimekubalika, hata kwa shingo upande. Am sorry, ni katabia kabaya sana lakini najiskia furaha kweli. Kuna kipindi Natamani ningesomea Sheria, kwenye cross Examination nipambane na upande wa mashtaka!

Sio kuwa convicted (kirahisi rahisi) without a reasonable doubt!

Hilo la kupenda kupindukia mbona wenzio ndio tunalilia? Penzi hilo...kutunukiwa thamani yake miye naijua, naitamani...
Sintotaka mwandani wangu apunguze,...yanini kupunguza ilhali roho inatamani?
Hebu acha huko!
 
Kaka mpendwa nisaidie, nisiwe mbishi basi. Sasa umependezwa na nini? Kutokuwa na mwenza au unashangaa ubishi wangu tu?
Kwanini tena uondoe quality yako nzuri ubishi ndio mzuri sababu mtu anakupa challenge kuliko kukubali yote unayosema, it means siku ukimkubalia inamaanisha ilo jambo ni perfect yaani hata wewe unalikubali
 
Reactions: Mbu

...LD sikutishi, ila nakwambia ni tabia mbaya madhalki mwenyewe haikupi amani.
Hapo penye red umenichekesha sana, ati?...ukipatia unachobishia unafuraaahi? ha ha ha...

Utaambiwa una hila, shauri yako.
Badilika bana, kubali kukosolewa bila kupinga.
 
BJ I wish ningewezakuwa kama wewe loh...........nahisi ni kutokana na kule nilikotokea..jamani hamjui inauma kiasi gani mtu kakukosea.....kwa makusudi, haombi msamaha wala hasawazishi kiutuuzima afu ikifika muda unasikia tu....geuka huku!! sawa una'swallow your pride' unageuka .......afu baada ya hapo haichukulii kama ile 'geuka'yako kama ni sehemu ya kumake up.........anaendeleza mnuno....mpaka siku tena 'babu' ana kiu ah.... acheni tu. I used to have a theory kuwa ...kama diplomacy imeshindikana, basi bibi/babu will do but unfortunately kwangu haijawork.

In addition Mbu...kuna yale ya
Mavazi, kazi e.t.c..........eti wakati wa uchumba kila vazi uvaalo wasifiwa, kazi yako wasifiwa afu baada ya 'pingu' .......nguo hazitaki na kazi waambiwa uache au ubadili!!!!Mi huwa sielewi kwa kweli, pengine nina matatizo!! ninaomba mnisaidie
 
...ooohh, pole BJ,
Lengo, nia na madhumuni yangu kwa thread hii ni kubadilishana mawazo kwenye....Samahani kama nimekukwaza, we'll come back to that.

Nimekusoma Mbu na kukuelewa!..halafu hujanikosea, hivyo don't be sorry bwana!...
btw kumbe wewe n mwepesi kuomba msamaha eeh?....thanks kwa mada nzuri!!

halafu fafanulia me ukiweza, aina gani ya malezi umekulia inayokupelekea kutaka kuwin arguments?
 
Reactions: Mbu

...sasa mwenzio atajuaje umeridhia au hujaridhia bana? Una ishara kama traffic lights? hebu kuwa mpole naweeee...Gubu hilo, lol!!!

....................Mbu jamani hivi kweli we ukimwudhi mpenzio, hutonote mpaka akwambie?? Hata kama sijasema (bahati huwa inachukua nguvu za ziada kuniudhi mie....mambo madogo nikilisema leo nimemaliza) .....na hapo ni kosa ambalo nimeshakuomba na kuomba kuwa sipendi husikii!!! Hapana kwa kweli nadhani as part of responsibilities ni kujua nini mwenzio anakipenda na kipi hakipendi ukiavoid.



Hapa mydia umeeleweka and I want to assure you kuwa kina kaka wengi sana huu ni ugonjwa wao......na nadhani wanawake wengi tunajisahau na kutaka kushindana katika mahojiano.............. mie marehemu bibi yangu alikuwa ananiambia kuwa ' mwanaume huwa haambiwi, hukumbushwa'...........kuwa kama mumeo/mpenzio hajafanya kitu/amekosea usimwambie.mpenzi unajua hapa umekosea, ulitakiwa ufanye a,b,c' bali mwambie ' Sweetheart, mbona unasahau kuwa kufanikiwa hili unatakiwa kufanya a,b, au c?.umesahau?' hata kama unajua kuwa hakuwa anajua........


Hilo la kupenda kupindukia mbona wenzio ndio tunalilia? Penzi hilo...kutunukiwa thamani yake miye naijua, naitamani...
Sintotaka mwandani wangu apunguze,...yanini kupunguza ilhali roho inatamani?
Hebu acha huko!

Mh we acha tu Mbu....... sitaki kabisa. Nina ugonjwa wa kusahau.............yaani leo umenikosea nipep siku tatu.nikiitwa mahakamani nitoe ushahidi wa kosa ulilonifanyia ..................sikumbuki!!!
 
Reactions: Mbu

...ha ha ha! ati geuka huku,...kwani ni rigwaride hilo?

Mwj1, kwakweli kwenye masuala ya kazi napingana vibaya sana na anayekushawishi eti ubadili kazi kwa ajili yake, Unless itakulazimu uhame nchi...na huko uendako una uhakika wa kupata ajira inayokidhi mahitaji yako. Lower self esteem ndio inamfanya mtu aanze kukwambia Oohh, kazi hiyo mimi siitaki ufanye,... It's not right.

Mnaweza jadiliana masaa ya kazi, maana kuna wengine ni workhaholics,...ukimuachia ndio imekula kwako.
Monday to sunday yeye kazini, akirudi nyumbani hoi taabani, nafasi nawe hana! ..Wengine hulala kazini ati, siku tatu....!
Binafsi, kama linaepukika simu za Boss ziwe na kiwango bana, sio wenyewe tupo kwenye kuliwazana mara simu; 'Oohh, kazi fulani haijisha bla blah!' matokeo yake sweetheart wangu anaishia kuwa miserable weekend nzima.

Nguo pia ni mashauriano bana, wote mnatakiwa kuwa flexible,...hivi Mwj1 ukinambia Mbu vikaptura unavyovaa haziendani na hadhi yetu halafu mimi nikanuna, itakuwa akili hiyo? Itanibidi nitafakari kwanza ukweli...Sawa nami nikwambie Mwj1 hizo leggings valia angalau gauni refu mama,...he he he!

Nimekusoma Mbu na kukuelewa!..halafu hujanikosea, hivyo don't be sorry bwana!...
btw kumbe wewe n mwepesi kuomba msamaha eeh?....thanks kwa mada nzuri!!

halafu fafanulia me ukiweza, aina gani ya malezi umekulia inayokupelekea kutaka kuwin arguments?

...Thx kwa kuelewa BJ. Unajua utotoni nilikuwa mtundu sana hali iliyopelekea kuchapwa mara kwa mara hata kwa yale ambayo nilikuwa naona sisthaiki kuchapwa. Mfano, nanunuliwa kigari cha kuchezea, siku ya pili nakuwa nimeisha kibomoa. Badala ya kupewa nafasi ya kujielezea, nikawa nakula fimbo!...Inaonyesha mother alikuwa keshachoka uharibifu wangu uliopitiliza...

Ubishi wangu ndio umeanzia hapo, ....yaani hata kama nimekosea, nisikilizwe pia. Sijakosea bure bure tu...mfano; vile vigari utotoni nilikuwa navibomoa kwa matarajio ya kuangalia kilichomo ndani yake ila ndio hivyo tena...kurudishia chap chap ilikuwa ngumu!
 

Mwj1...mimi ni mwepesi kuhisia something is not right nikishaona mwenzangu umekuwa cold ghafla.
Kama nimekuudhi kwa makusudi, nitatumia njia zangu nizijuazo 'kuua soo!'...shida ni kwamba, sio mara zote njia nitazotumia zitakuwa zinakidhi matarajio yako.
Mfano; Labda wewe ungependa nikukumbatie yaishe, wakati mimi nategemea nikikwambia "basi yaishe!" inatosha. Hapo inabidi uwe mwelewa.
Unless, from the beginning am sorry was always accompanied na a hug!

Kuna wale I forgive you means 'sex!,'...yaani bila kupewa haki yake anaona bado kanuniwa!
Huo nao ni mtihani ambao ningependa kuukwepa.

Apart from that,...huwa naomba clarification mtu amenunia nini,...zile za mnn, hamna kitu...huniachia maswali zaidi!
(pheeeeww, nimejishtukia naku address wewe as if wewe ni....hii kali)
 

Kaka mpendwa Mwanza hakuna kabisa, yani ni mimi tu peke angu.

Ila kuna mtu tulibrekiana hati enzi zile, sasa malalamiko yake ni kwamba mi ni mbishi. Na kweli nikijiangalia najiona mbishi halafu sipendi ujinga ujinga. Yani huwa siwezi kupotezea kitu yani. Sasa kale kajamaa kalikuwa kanaudhika kweli kweli.

Na mimi namuona anabisha mambo ya msingi. Au wakati mwingine nakubali yaishe lakini kesho narudi pale pale kwenye msimamo wangu.

Dah, kajamaa kakaona nakapotezea muda au sijui nakadharau, kaka nifanyia vitukooooooooooooooo, halafu kakaondoka.
 
Reactions: Mbu


eh........usijenfanya nikachukiwa bure..............

Afu huyo MJ (Michael Jackson) kwenye signature yako ..........Kwa nini hakuongezea One huko mbele lol
 
  1. -ve yangu kubwa sipendi kusimamiwa ninapopewa/ninapofanya kazi fulani iwe oficini au nyumbani,huwa ninaamini kama ni kitu kipya ukishanipa directives,siwezi kushindwa(niache uone kama nitashindwa,na nikishindwa si nitauliza?),sio unakaa nyuma ya mgongo wangu,unaamrisha"do this",no......no this way, mara that way,aaaugh.Yaani naweza kuacha kila kitu.Nikakutizama tu tena kwa hasira(sijui kwanini huwa naamini naweza, na ni mtu wa kujituma hasa)
  2. Ya pili,hata kama nimekosea,sipendi ushout huku ukiwaalert wengine how bad it was.If you do this "sitaapologize",and i will hate you.(Nieleze kosa kwa upole tena tukiwa mi and yu,hapo nitaomba msamaha mara mia).Hii husababisha wengine waone sipendi kuambiwa ukweli,kumbe ni approach waliyotumia imesababisha hivyo.
3. Nikiamini jambo fulani kuwa liko hivi,na ninalielewa vizuri na ushahidi ninao,hata ubishane nami jan-dec,sibadiliki.Zaidi sana nitaendelea kutafuta more evidence nikubadili wewe.

4. Mwepesi mno wa kusamehe,niko very understanding cha msingi muhusika awe mkweli,akiri na kuonyesha nia ya kubadlikika(hata kama nimeolewa then mume akaleta mtoto wa nje aliyezaliwa tukiwa ndoani),nitamsamehe.Nashindwa kuhukumu.
naona kama niko weak sana hapa,yaani moyo wangu ndivyo ulivyo mwenzenu sijui nifanyeje.

5. Mtu akiniudhi,awe ndugu,jamaa n.k (japo kuniudhi ufanye kazi haswaaa),nitakasirika,naweza kuwa na majibu ya mkato kwake ili nisitamke neno baya kutokana na hasira,huku najiuliza moyoni,"hivi hajui kama kaniudhi?",then baada ya muda,masaa n.k nikiona haelewi "nasamehe hukohuko moyoni",alafu naendelea na maongezi naye kama kawaida then ndio nitaweza mwambia kama aliniudhi na nimeshasamehe lakini hapo kumbuka nilishaumia ile mbaya "kimoyomoyo"

Nifanyeje niweze kubadilika,au nifanyavyo ni sahihi
 
Reactions: Mbu
eh........usijenfanya nikachukiwa bure..............

Afu huyo MJ (Michael Jackson) kwenye signature yako ..........Kwa nini hakuongezea One huko mbele lol

....nilitaka niweke MwJ (Michael "Wacko" Jackson) dhamira ikanisuta...lol!
close,....very close....!
 
Mimi kasoro yangu niko too critical. Nikisimuliwa story iso na kichwa wala mguu lazima nihoji. Na tabia hii najua kuwa ninayo kuna siku kuna dada alikuwa ana explain class kazi anazofanya na NGO fulani huko South America nikaona anatufunga kamba sikusubili amalize nikachombeza lecturer akaona mdada amechange akampoza akasema NK has been too provocative. Mme wangu uwa anachukia anataka nichukulie anachosema kama adithi za sungura. Ila kwa kuwa najua kasoro yangu ninajitahidi sana ku minimize.

Mme wangu kasoro yake ni kutokubali. Mfano mimi nina kumbukumbu sana naweza kumpa kitu afu baadae akakataa kabisa sijampa. Kumbe kasahau. Badala ya kusema sikumbuki kama umenipa au la yeye anakomaa. Huwa nakasirika sana. Imagine wewe memory yako iko certain kabisa kuwa umefanya kitu afu mtu anakana! Na siyo mara moja yani ni tabia yake sijuhi kwa nini akubali kuwa yeye ni msahaulifu. Maana mara nyingi anaishia kuumbuka lakini bado ajifunzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…