Chupi yako unaanika wapi.................?

Nakuunga mkono watu8. Nafikiri si jambo jema wala heshima kuanika chupi sehemu za wazi au nje! Utajisikiaje kuona chupi ya mama, baba, au hata dada yako au kakayako?

By the way, kama hautajali, hili jina watu8 maana yake nini?

ni kweli mkuu binafsi huwa naamini chupi ni vazi la heshima....
watu8 ni jina tu ingawa origin yake ni kikundi cha watu 8 tuliokuwa na nia ya kuanzisha kampuni kubwa lakini ndoto hizo zilizimika, so am trying to keep the name alibe so as the dream
 
Last edited by a moderator:
Utakua malaya, na utakua huvai chupi. Sasa kama huvai utakua unavua nini?
Ningejibu lakini najuwa unanitafutia ban, kwa ufupi muulize mom nyumbani, Zomba unamjuwa? jibu utakalopata fanya siri yako.
 

Kuanika chupi? Ndo nini hivyo? Chupi si kama toilet paper tu? Mi kila siku navaa mpya(joking)by the way. . .ni vizuri ziwe zinaanikwa juani, kuna uhusiano gani kati ya chupi na heshima? Labda ikiwa ina ukoko na imetoboka. . .mi hua naanika nje bila wasiwasi na brebs zangu ni all white.
 
una fungus kilo ngapi aisee? Manake chupi, soksi na taulo ni mitambo ya kuzalisha fungus! Na kila siku unapaswa kutumia taulo safi, sidhani kama unaweza. Hiyo ya taa za maabara za kuulia bacteria is too theoritical

binafsi nilikuwa najiuliza hivi huyu anatania ama ni kweli? hizo taa za kusterilize tu hata siye huku maabara tunakosa achilia mbali mafungu ya pesa yanayoelekwezwa kwenye maabara hadi tunatumia mabanseni bana sasa sijui atawasha stovu huyu.
 
Huku uswahilini tunakoishi haiwezekani maana choo/bafu ni vya kugombania.

nafahamu mkuu basi tuwe tunaanika hata ndani sehemu yenye mwanga kidogo...unajua kuna nchi hazina jua kabisa kila siku barafu mbona wanaanika nguo zao na zinakauka
 

Kuna jinsi mbili,hotelini huwa wanafua kwa kutumia washing machine.Kawaida kuna aina mbili za washing machine, kuna zile zinazokamua maji na kuiacha nguo nusu kukauka halafu kuna mashine za toleo la kuanzia mwaka 2010 zinazokausha kabisa yaan nguo ikitoka kwenye mashine ni kuipiga pasi na kuvaa.
Ukiacha hilo kuna aina ya taa ambazo huwa zinatoa mwanga wenye joto nguo humo ndani itakauka tu na hakitakuwa na ufundo wala ubichi wa aina yoyote.
 
Unaishi Tanzania hii! Imajini unachumba kimoja cha kuapanga na unafalia, usiku bed room, mchana sitting room, halafu hiyo nyumba inawapangaji 12, mnashare choo na bafu! Swali hii gumu!!

itundike hata juu ya feni itakauka vizuri tu
 
Bafu hili la paspoti size nyumba ya vyumba kumi na mbili?????
Taa inatumia solar au???

zinatumia umeme ndugu...binafsi bado naamini huwezi kosa mahali muafaka pa kuanika chupi ndani ya nyumba, hiyo chupi ni kipande cha gunia au turubai hata isikauke kiurahisi ndani.
 
Ivi Chupi bado zinavaliwa siku izi ?

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
kiafya zinatakiwa zianikwe juani ila kwa wanao share nyumba halahala na usafi usije ukafua ukaianika afu ukakuta nzi wameijalia!
 
zinatumia umeme ndugu...binafsi bado naamini huwezi kosa mahali muafaka pa kuanika chupi ndani ya nyumba, hiyo chupi ni kipande cha gunia au turubai hata isikauke kiurahisi ndani.

Mkuu kweli hujui makaazi ya Watanzania tulio wengi......unaongelea few of the mid-class na the upper ones........hebu fikiria mtu kama mimi mkazi wa Jangwani - Dar.......au Da Asha Di wa pale Mabwepande a.k.a.......the after math residential......au Lizzy wa Kishiumundu.......

Wote sisi tunaweza hii life unayoongelea hapa........?????? Wapi tuanike Chupi zetu?????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…