Chupu chupu jamaa afumuliwe marinda!

Nguvu moja

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2017
Posts
3,371
Reaction score
2,713
Ilikuwa hivi jamaa alikuwa anatembea na mke wa mtu ikawa ndio tabia yao ikifika mida ya saa mbili usiku jamaa wanapanga kukutana na mchepuko wake hoteli moja iliopo kariakoo kwa ajili ya kupata dinner.
Wakitoka hapo wanaondoka maeneo mengine mbali na hapo kariakoo, kwa sababu huo mchepuko wa kike unaishi maeneo ya kariakoo mtaa wa lindi... Na isitoshe mume yeye na mumewe walikuwa wanaishi kariakoo mtaa wa mhonda, hila walikuwa na kutokuelewana mke na mume ikabidi mke arudi kwao mtaa wa lindi hapo.
Ndio mke wa mtu mama wa kizaramo akatafuta mchepuko wake... Akampata huyo jamaa lazima ikawa saa mbili usiku wakutane wapeane dinner wakitoka hapo wanachukua usafiri wa daladala wanaenda kulala guest moja temeke stereo.. Ikawa ndio tabia yao sasa za mwizi 40 jamaa mwenye mke.
Wapambe wakamwambia na kumweleza mwenye mke na jamaa mwenye mke ni muhehe wa iringa.
Jamaa akawapanga watu wa kumfuatilia mkewe na jamaa kila hatua wakikutana na huo mchepuko wake sasa ikawa hivi juzi, jamaa yule mgoni kaenda kuuchukua mchepuko wake wakaenda kula walivyomaliza kula kumbe kuna mtu akawa anawafuatilia bila wao kujua hatua moja baada ya nyingine walipomaliza kula wakapanda gari kuwapeleka temeke stereo kwenye hiyo guest wanapolala, bila kujua wanafuatiliwa na mtu nyuma yao yule jamaa alipopata uhakika jamaa kaingia guest chumba namba furani... Yule bwana akampigia simu mwenye mke aje kufumania. Jamaa wakabeba mapanga visu wakawa wanakuja eneo la tukio wafumanie.
Lakini jamaa akaamua kupitia kituoni atoe taarifa kwanza alipomaliza kutoa taarifa kituoni akapata askari wa kwenda nao mpaka kwenye hiyo guest saa saba usiku walipofika kwenye hiyo guest jamaa wakamgongea mlango wakamkuta kweli na mchepuko wake wakahojiwa kidogo pale wakachukuliwa kwenda police kufika kule mke akaulizwa kwa nini unafanya mambo hayo haikadhalika wewe ukiwa mke halali wa mtu yule mama akajibu bila wasi wasi kama hivi mimi huyo baba watoto wangu nimezaa nae watoto wawili nina mgogoro nae mwezi wa tatu huu anihudumii mimi wala watoto wake mie nifanyaje hata unyumba anipi mwezi wa nne huu na mimi najisikia hamu..basi kutoka pale jamaa ikawa mwisho wao na kuachana na mke wake.
 
mbona hakuna viashiria vya mtu kufumuliwa rinda au mimi ndio sijui kusoma vizuri
 
we mwanaume wa dar savanah ya nn........watu tunachanganya konyagi kubwa na konyagi ndogo.....
 
Sasa mke aliyerudi kwao unamfuatilia wa nn?!


Kuna watu hawana akili kbs
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…