Chura anapenda sana maji, dhat is why alishindwa kuruka kwenye sufuria hadi akafia pale

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Posts
7,872
Reaction score
9,263
Chura anapenda sana Maji.

Tuna penda sana kazi asikuambie mtu, tunapenda sana tuonekane tuko ofisini hata kama kazini ni kugumu namna gani potelea mbali si niko kazini?


Tunapenda sana mtaani na ndugu na jamaa wanapo ona tuko kazini kwa watu tunatumika.

Sisi ni kama chura anaye penda maji na analinga sana akiwa kwenye maji yake bila kujalisha hayo maji yana mamba, sumu, tope, kinyesi na kadhalika.


STORY YA MAJI YA MOTO

Chura baada ya kuwa kwenye chombo cha maji ya Baridi na kile chombo kuwekwa jikoni.Chura hakutaka kuruka kwa sababu zifuatazo:

1. Chura anapenda maji vibaya mno so haijalishi yana kinyesi, sumu au ni ya aina gani,

2. Chura alijua anaweza pambana na mazingira yoyote yale pale.

3. Chura ailijua mwishoni kama ikishindikana basi ataruka.

KILICHO TOKEA
Chura alikuwa anajibadili kila maji yalivyo pata moto. Chura alikuwa ana adjust joto la mwili wake ili kupambana na Maji yale.

Mwishoni baada ya joto la maji kuwa kari sana chura aliona aruke ila alishindwa.

KWA NINI CHURA ALISHINDWA?
Kwa sababu alikuwa ameisha tumia nguvu na muda mwingi ku adjust hivyo hakuwa na nguvu za kuruka.


SISI WAFANYAKAZI SASA

Wafanyakazi tunapenda sana kazi asikuambie mtu, ni sawa na chura na maji kwamba hata kama kazini nitatukanwa, nitagombezwa kama mtoto mdogo na ilihali nyumbani mimi ni Baba au mkuu wa nyumba.

Niko tiyari kuishi na kufia kwenye kazi bila kujalisha mazingira ya kazi mimi ilimuradi Mtaani na Ndugu na jamaa na marafiki wanajua niko kazini.

Chura analinga akiwa kwenye maji. sasa na Mimi nalinga kwa sababu niko kazini haijalishi nalipwa shi ngapi au natukanwa vipi au nagombezwa vipi.

KAZI INAPO KUWA NGUMU NA.MSHAHARA MDOGO.

1. Ataenda kusoma kama ni Degree basi ataongeza ya pili.

2. Atahama kazi na kwenda kutafuta lazi kwingine.

3. Atalilia over time.

MWISHONI MWA SAFARI

Baada ya kutumikishwa kwa miaka 40 au50 sasa atasatafu. Atastafu make kule haihitajiki tena na sio productive.

BAADA YA KUSTAFU SASA

Ataanza Ujasiriamali, atakuwa bise sana na kilimo au Duka wengine wananunua Daladala na wegine TOYO na wengine wanaenda kwenye Madini.

TOO LATE

Hapa inakuwa ni sawa na chura make chura alikuwa na nguvu za kujamp pindi akiwa na nguvu ila alisubili hadi nguvu ziishe na kujaribi kuruka na akashindwa na kufa.

UKISTAFU mara nyingi nguvu zinakuwa zimeisha almost 75% ya nguvu zinakuwa zisha tumiwa na wenye akili na marisk taker, sasa unabakia na 25% hii ni nguvu ya kukuwezesha kula na kuongea na si nguvu ya misuko suko ya biashara.


Ukistafu unatakiwa upumzike na si uanze kutafuta pesa. Inakuwa too late sana tena mno.

Ukistafu kama ni kufuga fuga Ng'ombe wako kwa ajili ya kunywa maziwa au Duka mbele ya Nyumba yako kwa ajili ya usikae mpweke ila si kwa ajili ya kutafuta pesa.


MWISHO

Wacha kuwa kama chura kwamba alisubili hadi wakati ambao ni too late ndo aruke kutoka kwenye Sufuria la.maji ya moto.

Wacha kungoja ufukuzwe kazi ndo uanze ujasiriamali.

Wacha kungoja upunguzwe kazi

Anza ukiwa na nguvu kamili bila juwa na aina yoyote ya Msongo wa mawazo.

By
Chasha Farming




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawajua matajiri nchi hii waliokamata pesa kwenye lste 50's zaidi ya 7.So habari za Age na mafanikio sometimes hazina direct correlation kiviile.
 
MKUU UMEONGEA UKWELI, NIKUHAKIKISHIE TU, WAMEUSOMA WENG UZI HUU NA HUKO WALIKO WAMEPATA STRESS ZA GHAFLA UTADHANI JAMBO HILI NI GENI KWAO.

TATIZO MINDSET

UJUE IMEFIKA HATUA JAMII YETU YA KITANZANIA 'KUJIAJIRI' HAWACHUKULII KAMA NI AJIRA

WANATAKA UITWE MHASIBU WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NANYUMBU WAKATI UNALIPWA 750,000 BAADA YA MAKATO INABAKI 500K

HATA KAMA UJASIRIAMALI UNAKUINGIZIA MILIONI 5, WAO HAWAELEWI WANAONA UMEISHIWA MIPANGO NA WENGNE WANAULIZA SASA ULIKUWA NA MAANA GAN YA KUSOMA WAKATI HAUNA KAZ?

YANI HUKO TZ KUAJIRIWA NDIYO AJIRA ILA KUJIAJIRI SIYO AJIRA
 
Nilikutana na mwalimu wangu wa primary..aliniambia pamoja na kusoma kote huko umeamua kufanya biashara?
Mindset ndo tatizo la wengi, sijui wanadhan biashara ni kwa ajiri ya nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Embu acha kutuchoma na maneno yako bwana.....si tushazoea kusifiwa na kutiwa moyo tu
 
sindano imeniingia haswa,,,hebu nisaidie mawazo ya ujasiria mali wakufanyaa please
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…