Wanajamvi Mh. Samweli Sita karudi kwenye nyadhifa kama aliyokuwa nayo msimu wa kwanza wa serikali ya awamu ya nne, akiwa kama Spika wa bunge. Tofauti ipo kwani sasa ni Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba. Je, yeye kama chura (mzoeufu kwenye kiti cha kuongoza bunge aliyepewa tena nafasi hiyo) je ataweza kuzuia mapendekezo ya chama chake CCM yanayopingana na rasimu ya katiba, yani mkoromo wake kama chura utamzuia tembo kunywa maji (CCM)? au ni business as usual! Usanii ule ule tulionao kwa wanasiasa wa chama tawala? Napata wasi wasi kama mapendekezo ya wananchi yatazingatiwa au mapendekezo ya chama tawala ndo yatapewa kipaupendele. Manake rasimu haikubaliki na chama tawala, yaani mawazo ya wananchi sio ishu kwa chama tawala CCM. Kazi ipo.