Citizen TV ya Kenya imeripoti Rais Samia kawaachia wafungwa 23 wa kisiasa. Ni akina nani wafungwa wa kisiasa?

Citizen TV ya Kenya imeripoti Rais Samia kawaachia wafungwa 23 wa kisiasa. Ni akina nani wafungwa wa kisiasa?

mr gentleman

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
3,222
Reaction score
4,689
Televisheni ya Citizen ya Kenya imeripoti kuwa Mama Samia ametoa maelekezo wafungwa 23 wa kisiasa waachiwe huru.

Je, Tanzania tuna wafungwa wa kisiasa?

Ni kina nani hao wafungwa wa kisiasa anaowazungumzia Mama Samia?

Au Citizen wanamchafua rais wetu?

=====

Serikali ya Tanzania yakanusha kuwa na Wafungwa wa Kisiasa. Serikali imesema rais hawezi kuingilia uhuru wa Mahakama.

Zaidi soma: News Alert: - Dar: Serikali yakanusha kuachia Wafungwa wa Kisiasa, yasema Tanzania haina mfungwa wa kisiasa

Kenya wamekuwa vyombo vya habari kuliko msemaji mkuu wa serikali. Siku zoto raisi hawezi semewa nchi ya watu mpaka nisikie nchini mwangu
 
Mdude kakutwa na unga ndani kesi yake sio ya kisiasa.

Lakini je Mdude kaachiwa?
Kwani kwa akili zako unadhani wafungwa wa kisiasa files zao zinasoma kuwa wameshitakiwa kisiasa?

Unapewa kesi yoyote ile wanachofanya ni kukulia timing wakukamatie wapi.

Unaweza pewa kesi ya ulawiti, ubakaji n.k ila nyuma kuna political influence.
 
Kwa hiyo Mdude kaachiwa?
 
Back
Top Bottom