CJ;Futa utaratibuwa session mahakama za juu unachelewesha haki kutendeka na kuonekana

CJ;Futa utaratibuwa session mahakama za juu unachelewesha haki kutendeka na kuonekana

nyundo2017

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2017
Posts
1,439
Reaction score
861
Hongera CJ

Napenda kukushauri huu utaratibu wa "session" uufutilie mbali kwani unachelewesha haki za raia.
Unakuta majaji wapo na wanalipwa mishahara yao kila mwezi lakini kesi haziendi wakisubiri session na session zenyewe hazifanyiki hadi kuwe na pesa za posho za vikao vya majaji,mbona mahakimu wanaendesha kesi kila siku hawasubiri vikao?

Kero kubwa iko divisheni ya kazi mahakama kuu ambako majaji wengi wanaishi dar es salaam hadi vikao vifike na hela zipatikane ndiyo wanaomekana vituoni,je hii ni sawa?

Wafanyakazi wengi wanaachishwa kazi zao kwa hila hasa serikalini pasipo sababu za msingi au kufuata taratibu,anaenda CMA ambako ucheleweshaji wa kesi ni mkubwa sana pasipo sababu za msingi akitoka hapo ni rufaa kama kuna upande haujaridhika sasa huko ndiyo miaka kibao nenda rudi,nenda rudi kisa vikao havijaanza hamna hela za vikao vya majaji.

Je waliajiriwa kwa kutegemea posho zaidi?

Nawasilisha kwako.
 
Back
Top Bottom