SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Sikupata wasaa wa kuangalia game ya marudiano ya Zambia vs Lesotho katika mashindano ya kutafuta kufuzu AFCON. Katika mechi hiyo Zambia walishinda 2-0.
Katika mechi hiyo, kiungo wa Simba, Clatous Chama aliingia kipindi cha pili dakika ya 80 na kucheza kwa takribani dakika 10+. Takwimu nilizopata zinaonyesha aligusa mpira karibia mara 20 akitoa pasi mbalimbali za maana kwa wenzake.
Leo nilipoangalia highlights za mechi hiyo, ilionyesha wakati Chama akiingia. Huwa si kawaida highlights za mchezo kuonyesha pale mabadiliko ya timu yanafanyika unless mchezaji anayeingia ni mchezaji mkubwa. Hilo ni jambo la kwanza nililochukua.
Baada ya hapo highlights hizo kwa bahati mbaya hazikuonyesha sana movements za Chama ila baada ya mchezaji mmoja wa Zambia kuchezewa rafu, mtangazaji alitoa comment moja akisema "toka Chama ameingia katika mechi hii amechezewa rafu nyingi" akiongezea kuwa "kila mchezaji anayekuja kucheza katika mechi hizi anaombea arudi salama katika club yake bila majeruhi".
Kwa hiyo nililochukua kutoka highlights ile ni kuwa uwezo wa Chama unajulikana vizuri Africa hii na Lesotho walijipanga kumzuia kwa njia zote asiweze kufurukuta.