Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mshambuliaji kinda mzoefu wa miaka 20, Clement Mzize, ameonekana kuwa hatari katika kikosi cha Yanga, akionyesha kiwango bora katika mechi za kirafiki na mashindano.
Sifa zake za uchezaji zimemfanya kuwa mchezaji wa kutegemewa, na sasa matumaini ya Tanzania kufuzu Michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Morocco mwaka 2025 yanaweza kuwa mikononi mwake.
Ikiwa kocha wa Taifa Stars, Hemed Suleiman 'Moroco', atampa Mzize nafasi ya kuanza kwenye mchezo wa leo dhidi ya Ethiopia, ambao utachezwa saa 1 usiku kwenye Dimba la Benjamin Mkapa, kuna uwezekano mkubwa kwamba kijana huyu atakuwa na mchango mkubwa katika ushindi wa Tanzania.
Mzize ana uwezo wa kupeleka mashambulizi ya kasi na kushambulia kwa ustadi, jambo ambalo linaweza kuwa silaha kubwa dhidi ya Ethiopia.