Clement Mzize amebeba tumaini la Stars kufuzu AFCON 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mshambuliaji kinda mzoefu wa miaka 20, Clement Mzize, ameonekana kuwa hatari katika kikosi cha Yanga, akionyesha kiwango bora katika mechi za kirafiki na mashindano.

Sifa zake za uchezaji zimemfanya kuwa mchezaji wa kutegemewa, na sasa matumaini ya Tanzania kufuzu Michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Morocco mwaka 2025 yanaweza kuwa mikononi mwake.

Ikiwa kocha wa Taifa Stars, Hemed Suleiman 'Moroco', atampa Mzize nafasi ya kuanza kwenye mchezo wa leo dhidi ya Ethiopia, ambao utachezwa saa 1 usiku kwenye Dimba la Benjamin Mkapa, kuna uwezekano mkubwa kwamba kijana huyu atakuwa na mchango mkubwa katika ushindi wa Tanzania.

Mzize ana uwezo wa kupeleka mashambulizi ya kasi na kushambulia kwa ustadi, jambo ambalo linaweza kuwa silaha kubwa dhidi ya Ethiopia.
 
Jiandae kuwa disapponted
 
We are done for alisikika mzungu mmoja wa buza. Anyway namuunga wa mbagala mkono hoja
 
huyo hemedi ni kocha wa hovyo kabisa,hafai hata kuwa kocha wa nakapanya fc
 
Msimpe dogo pressure na litimu letu lisilo na mipango🚮🚮
 
Kikubwa awe makini asije akaumia na kuigharimu club yake ambayo ina mashindano muhimu zaidi.
 
Shida ndio inapoanzia hapo,mnambebesha mzigo mzitokijana mdogo aingie uwanjani na mawazo lukuki,wachezaji wetu kujipambanua wanapo kuwa wao kwa wao huwa ni ngumu ngoja tuone.
 
Mnampa majukumu mazito, mnasahau kule Yanga kazungukwa na mafundi.
 
Duuuh sio kwa uchezaji huu wa hawa vijana..timu ya Taifa isi wa include hawa watu Wa yanga na Simba ni upupu..hasa wa yanga ndo upupu zaidi...
 
Hawezi, labda Azizi Ki acheze.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…