Clement Mzize Kutua Ufaransa Klabu ya Olympic Marseille kwa Majaribio

Clement Mzize Kutua Ufaransa Klabu ya Olympic Marseille kwa Majaribio

Kurunzi

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
9,753
Reaction score
10,747
KLABU ya Yanga imepokea mualiko wa mshambuliaji wake kinda, Clement Mzize ambaye anatakiwa na klabu kubwa ya Olympic Marseille ya Ufaransa.
Mkurugenzi wa ufundi wa Yanga Mwinyi Zahera amesema tayari Marseille wameshatuma mualiko wa kinda huyo kutakiwa kwa majaribio ya wiki mbili yatakayofanyika nchini humo.
Marseille ambao wamemuona kinda huyo katika Mashindano ya soka la vijana chini ya miaka 20 ambapo mshambuliaji huyo alionyesha kiwango bora akifunga mabao 7 na kuwa mfungaji Bora.
Tayari Yanga imeshapokea mualiko wa Clement ambaye anasubiri kupata visa tayari kwa safari ya nchini Ufaransa katika majaribio hayo.
Yanga imemjumuisha kinda huyo katika kikosi chao cha msimu huu ambapo katika mechi tatu ambazo Yanga ilicheza za kirafiki kabla ya ligi kuanza alipachika mabao mawili wakati Yanga ikiichapa Friends Rangers kwa mabao 9-0.
"Huo mualiko upo klabuni viongozi wanaufanyia kazi nafikiri katika majaribio hayo atafanikiwa kwa kuwa nimekuwa naye naona ubora wake kwa umri wake Marseille hawataweza kumuacha,"amesema Zahera.

"Ni mtoto hodari sana ana nguvu na anajua kufunga naona jinsi Tanzania inapata shida katika kuwa na wafungaji wazuri,huyu Clement kama atatunzwa vizuri na kuendelezwa na yeye mwenyewe kujitambua atakuja kuwa mtu Bora katika taifa hili
 
Taarifa ilikuwa propaganda ya toka mwezi wa 8 huko,,hayo ni maneno ya zahera tumeshayazoea tuliwahi kuambiwa ambundo anaenda Aston Vila
 
Tatizo ni nini klabu za Tanzania kutowapa dakika nyingi za kucheza ktk ligi au kimataifa zinapokuwa na wachezaji 'madogo' kama Kelvin John, Clement Mziza hata Mbwana Samatta alipokuwa dogo hawapewi nafasi kama ilivyo Genk KRC kwa Kelvin John, Olympic Marseille kwa Clement Mzize au TP Mazembe wakati Mbwana Samatta akiwa dogo.

Kwanini ma-father wa miaka mingi kupitiliza timu kubwa Tanzania ndiyo wanapewa nafasi ktk ligi halafu ma-father haohao timu yao wakichezeshwa kimataifa ulimi unatoka nje maana wanakutana na 'madogo' wa timu zingine za nje ambapo wanaamini ktk kuwapa wachezaji hata awe na miaka 16 mradi anaweza huaminiwa kucheza kikosi cha kwanza cha timu iwe klabu au timu ya taifa.

Tujiulize kwanini Tanzania tunawabani 'madogo' hadi wafike miaka 28 ndiyo wapewe nafasi kikosi cha kwanza ? Ni kwa faida ya nani klabu zetu na timu ya taifa kupendelea wazee waliochoka?
 
Back
Top Bottom