Click Farms: Njia mpya ya kuwatapeli watu katika nchi zenye mishahara midogo

Kingsmann

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2018
Posts
4,805
Reaction score
17,850
Click Farms/Mashamba ya Kubofya/Kubonyeza.



Haya ni maeneo, hasa katika Asia, ambapo matapeli "hufanya kazi" kwenye mamia ya simu za rununu kwa wakati mmoja kwa malipo duni.

Bosi wao ni "mkulima wa kubofya au kubonyeza" ambaye ni kama "bwana shamba."

Matapeli hawa hucheza video kwenye tovuti zinazolengwa, hujiandikisha kwa ajili kupata jumbe pepe(emails) na majarida(newslatters) na kusambaza likes za uongo.

Your browser is not able to display this video.


Wanaunda trafiki bandia kwenye wavuti kwa kifupi, Wateja wa tovuti hizi basi wanaamini kuwa utangazaji wao umeenda vizuri kumbe ni mtu mmoja anacheza na mamia ya simu.

Huwezi kutambua ulaghai huo, kwa sababu matapeli hawa wanaobofya wanaonekana kuwa na tabia kama watumiaji wa kawaida.

Tukae chonjo huko mitandaoni, usiamini sana kwenye likes na views maana kwa sasa kuna "Mashamba ya Views, Likes n.k."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…