MCHONGANISHI
JF-Expert Member
- May 28, 2011
- 372
- 364
Jamani ndugu zangu naomba mnisaidie katika mimi na wajasiriamali wenzangu tulifanya kazi fulani katika halmashauri ya Meru Arusha na wakati wa malipo tuliwapa account ya kikundi chetu ili watulipe, account hii iko CRDB na hadi leo pesa zilikuwa hazijaingia katika account yetu. Asubuhi nilienda katika ofisi za halmashauri na kweli akinionyesha katika decument zao kuwa wameshawaagiza NMB Bank tangu tarehe 25 mwezi huu wawalipe CRDB kutoka katika account ya halmashauri ili watulipe, na akaniambia itachukua siku kadhaa. Huku wenzangu tayari wakinijia juu wakihisi nimewadhulumu, na mimi pia simuamini huyu mhazini wa halmashauri je hii kitu ni kweli? na kama ni kweli huchukua siku ngapi????? tafadhali naombeni msaada wenu