Cloud 112

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Jina lake halisi anaitwa issa mussa,anafahamika zaidi kwa jina la cloud.huyu ni muigizaji wa long time kidogo,aliwahi kushiriki michezo ya kuigiza apo awali kabla ya kuamua kujikita kwenye filamu.movie yake ya kwanza iliyomtambulisha vyema kwenye ulimwengu wa filamu inaitwa SABRINA,kwa aliyewahi kuitazama hii movie,ni kati ya movie iliyowahi kutikisa miaka hiyo.tokea apo tukaanza kumuona kwenye movie mbalimbali mpaka apo alipoamua kumiliki kampuni yake binafsi ya movie.hizi ni baadhi ya movie ambazo ameziandaa bwna mkubwa na kuweza kufanya vizuri sana sokoni kuna KINYONGA,TOBA,TIFU LA MWAKA,FUNGATE,BASILISA,TRIPPLE L na nyingine nyingi tu,kwa kifupi huwezi kuwataja waandaaji wa movie za kibongo bila kulitaja jina lake,anafanya vizuri kwa kweli,kama unataka kuthibitisha hilo kanunue TOBA,nimeona kaingia jamii forum,tofauti na mastaa wengine ambao tupo nao humu na wameamua kujificha Identity zao kwa sababu wanaozijua wao,swali langu kwa cloud ni hili,kwa nini umeamua kuji expose jamii forum na nini lengo lako haswaa la kuingia humu??,nitafurahi kama nikijibiwa na mwenyewe cloud,maana najua akina ufito kwa kudandia basi kwa mbele....
 
unajuaje kama ni yeye mkuu..

I know him kwa kupitia movie zake nyingi tu,pia uwa nafuatilia mahojiano yake mengi najua anavyoongea,najua ni mtu wa aina gani,kama sio yeye kuna maswali kadhaa nitamuuliza ambayo yako deep sana,nitajua kama ni yeye na nitawaambia
 
Kama kweli ni mwenyewe basi atuthibitishie hapa ili tuzijadili filamu zetu kwa kina na vina! Wengine sisi tunapenda sana kuangalia filamu za bongo lakini mapungu yake yanatufanya kushindwa kuvumilia kuangalia hadi mwisho wa filamu husika! Sina matatizo na wasanii, tatizo langu kubwa ni kwa waandishi wa story/scripts!! Hawa ndo tatizo....kuandika si kama kuigiza! You can train a person to act but to write, ama uwe na kipaji hicho au upate formal training! When you've THE BANG SCRIPT, unaweza hata kuchukua watoto wa mitaani ukawaelekeza what to do(provided director anajua kazi yake) na ikatoka bonge la movie!! In contrast, unapokuwa na WORST SCRIPT, hata ukichukua waigizaji na Directors wakubwa kutoka Hollywood, filamu husika itakuwa mbovu unless Production Script iwe completely different with Spec Script!

So, kama Clouds yupo hapa, welcome brother ili tusongeshe game!
 
Cloud karibu tuwapige sindano za moto tusonge mbele!
 
Kama ni yeye atokee tumswalike

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Yeye yupi? Aje aje!! Mnamaliza keypads hata sauti haitoki nje ya vi-electro-device vyenu,HAWASIKII
 
warumi kwa maelezo yako hapo juu yatosha kusema wewe ni mdau na mfuatiliaji mzuri wa Tasnia ya filamu hapa nchini.

Yawezekana nawe ni mmoja wa wasanii/watayarishaji wa filamu ambao mpo hapa JF lakini hamjaamua kutumia majina yenu.

Cloud 112 amefanya kitu kizuri kujiunga na JF, na nina thubutu kusema ni ujasiri mkubwa na pia maamuzi yake ni sahihi kwani hii itamfanya kuwa karibu na wadau wa tasnia ya filamy ambao wangependa kuchat nae na kumuuliza maswali kama hivi alivyofanya warumi na wengine kwa lengo la kuleta mapinduzi ya kweli ya Bongo Movie.

Mwisho niwathibitishie kua Cloud 112 ndio yeye halisi kwa maana ya actor na mtayarishaji wa Bongo movie, tunafahamiana sana na Cloud na nimewasiliana nae kuthibitisha hili. Na yeye atakuja kujibu maswali yenu hapa!
 
Last edited by a moderator:

Tunashukuru kwa taarifa nzuri,ila angekuwepo mwenyewe ingekuwa vizuri zaidi,mimi sio msanii,wala muandaaji wa filamu au kujishughulisha na mambo yeyote ya filamu,japokuwq napenda kufanya hivyo,mimi ni mdau wa movie za apa kwetu tanzania,japokuwa wengi hupenda kuziponda movie za nyumbani,kwangu ni tofauti nimezaliwa tanzania na ni lazima tujifunze kupenda kazi za watanzania wenzetu,tulipotoka ni mbali kuliko tunapoelekea,so mpaka hapa tulipofikia ki ukweli tumepiga hatua,japokuwa bado improvement zinahitajika,na wakuleta mabadiliko ni mimi na wewe,so lets join hands ili tuweze kufanya mabadiliko kwenye tasnia ya filamu apa nyumbani..
 
Last edited by a moderator:
kama cloud hupo hapa nijibu toka ndani ya nafsi yako, je ulihusika kumuua yule Zuweina??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…