Clouds: Acheni kufagilia upuuzi - wewe Diva - Loveness Love unajiaibisha....

..........Udhaifu wa kipindi unasababishwa na nani kama sio huyu mtangazaji? Wewe bana hebu soma vizuri thread na kuelewa.

Itakuwa wivu tu wa kike...GPL wanaweka picha za uchi kwenye magazeti yao...sijaona thread yako...mwana!
 
Unaposema eti saa nne watoto hawajalala, wewe una tatizo na lazima kwenye malezi ya watoto wako ni una kasoro, usimzingizie Loveness kabisa, jirekebishe, angalia watoto wanatakiwA kulala saa ngapi na kwanini waiskilize radio saa nne usiku?

Jichunguze kwanza kabla hujamlaumu Ms DIVA. Malezi kwa watoto wako ni mabovu na ni wewe ndio unaharibu watoto wako.
 
hapa haimaanishwi watoto as watto wadogo ........watu chini ya miaka 16 wanachukuliwa kuwa ni watoto kwa sheria za tanzania na hawatakiwi wafanye mapenzi let alone kujua position gani zinawafanya wa cum upesi!

time hizo ndio wanafunzi huwa wanasoma, akiwa amefungua redio ndio ajifunze vitu hivyO?

tanzania tunakoelekea siko hata kidogo .................akili zetu zote ziko kingono zaidi na hakuna sheria zinazobana hivi vitu.
 
Hawa watangazaji wa siku hizi ni lazima itafutwe namna ya kuwadhibiti. Wanatuharibia sana watoto wetu.
 
cheap labour.Kusaga anataka watu wakuwalipa mshahara kiduchuuu.wamepewa sana maonyo na tcra lakni inaonekana ni vichwa ngumu.huyo diva na power breakfast ndo vipindi unprofessional kabisa.hii radio haina hata mhariri wa vipindi yaani watu wana free style tu na ndo mana kuna ujinga lukuki
 

Kwani ukiambiwa mtoto ni lazima awe na miaka 2? Hata miaka 17 naye ni mtoto Ebo!! wewe wa wapi wewe? Yani unashabikia watoto wetu kuharibiwa na mafundisho ya kipumbavu?

Mie nasikitika sana kwa habari hii ya CLOUDS.

Vijana wengi wametekwa sana na hii redio, kwani hata mdogo wangu huwa habanduki kusikiliza kumbe ndio upuuzi huo anaujaza kichwani.
 
Hii dunia imeshabadilika sana ...watu hawana haya ,watu hawamwogopi mungu. aadili yamemomonyoka ..hata hiyo Discussion ni mojawapo ya maadili kupoteza mkondo wake .....

Wanashabikia Ujinga?

Hivi na huyo dada L ni The Diva wa ukweli au???
 
Kama mmesikiliza.. andikeni barua kwenda kwa Waziri wa Habari na msema kilichosema, kipindi gani na mada gani.. wenzenu hapa mtangazaji akitumia neno la "F" kwenye prime time.. barua zinazoingia huko FCC hadi wanakoma. Au mmesahabu mambo ya Janet na vazi lake? Wazazi wa Tanzania labda wanafikiria ndio maendeleo yenyewe hayo wote wanatikisa vichwa pembeni. Tafuteni namba ya Waziri wa Habari mpigieni au mtumieni txt hadi atoe tamko..na kuchukua hatua.
 
Nilisikiliza redio moja ya South Africa kila baada ya muda fulani wanalazimika kupiga promo ya kuelezea kama kuna lugha isiyo sahihi imetumika waripoti katika chombo kinachosimamia maadili ya utangazaji...huku kimya naamini wananchi wa kawaida hawajui walalamikie wapi.
 
My next question would have been.. hivi huyu binti kama ana boyfriend anayemsikiliza saa hizi..itakuwaje?
kumbeee!!
HATA HIVYO HIYO SI EXCUSE YA KUTUMOMOMYOLEA MAADILI YA WATOTO.

Duh heri angekuwa nae huyu anamegwa na kuachwa ana stress za kuto pata mme wa kumuoa.
 
Tatizo la msingi tunalokabiliana nalo kama taifa hivi sasa ni Mmomonyoko wa maadili ambao kwa kiasi kikubwa umeletwa na "Utandawazi".

Matokeo yake tunashindwa kuchagua zuri na baya bila kujua ya kwamba vyombo vya habari ni moja ya vyanzo vikuu vya kumomonya maadili ya taifa lolote lile.Mbaya zaidi tumefikia hatua ya kuabudu "Ngono" kama kitu cha kawaida tu kisichokuwa na miiko.

Sasa tunarithisha vizazi vijavyo maadili ya ajabu ambayo yatawasumbua sana kwa siku za baadae.Hivyo hata wanahabari wetu inawabidi kubadilika na kuibadilisha hali hii hapa ilipofikia ili tuweze kuishi kistaarabu.
 
..
hata ningekuwa peke yangu,nasikiliza bado nisingependa kuona mtu anaongelea mambo yake ya faragha!,hayanihusu kabisaa....isitoshe wana mambo kibao ktk jamii ambayo wangeweza kuyazungumza!
ni ujinga/utoto i hope..watajirekebisha..
 


Ndugu yangu..hebu mpe somo huyo ndugu anayebwabwaja biLa hata kuwa na uwanda mpana wa uelewa. Mwambie atafute definition ya mtoto ni nini ndipo aje hapa kutukana watu na malezi.Inaelekea ni walewale waliolelewa ovyo ovyo..ndio maana anavutika sana na mambo ya LL.
Anadhani mtoto ni yule anayevaa pampers na bibb shingoni!
 
Kwa kweli haka kabinti nadhani ni hamnazo. Siku moja alikuwa na kaka mmoja sijui jina lake nani lakini baada ya kupiga domo wakaanza kuongea ati twende kufanya sex! Kaka anasema wafanyie hapo hapo, binti (Loveness) anasema waende jikoni. Upuuuzi mtu redioni tena live! Aibu kubwa, sijui kama babake na mamake wanamsikilizaga au la.

Nahisi huenda hata hilo jina la Loveness Love si la kwake anajificha maana babake akisikia anatajwa nadhani anaweza kumlaani.
 
mm nafikiri tatizo ni wamiliki wa redio wenyewe wanawasapoti sizani kama wanawazuia kufanya upuuzi wao wa kuvunja maadili
 
Huyo anayejiita Loveness aka Diva ni mtoto wa Kamanda wa vijana CCCCCCCCCCCM wa mkoa wa Kagera na mfanyi-biashara maarufu Dioniz Malinzi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…