Ni aibu kwa level ya Radio kama Clouds kuwa na matangazo yanayohamasisha watu kubet kila dakika. Ubunifu wa kupata mapato umeisha wamebaki kutegemea Buku Buku za wasikilizaji. Clouds imekua radio ya ajabu sana kwasasa. Kama hali imekuwa ngumu wauze hisa tu ili wapate mwekezaji mwingine.
Tunafanya mambo kwa kutegemea wachezeshaji wengine ili tupate faida ambayo hatujui hata kama tutaipata (ingawa kwa past events na tabia zetu ni kwamba tutapigwa); Tunaishi kwa mategemeo ambayo mathematically the odds are not on our side....
Clouds yupo kazini (kwenye betting ukitaka ushinde either uwe mchezeshaji au wafundishe watu jinsi ya kucheza wewe pesa yako inakuwa guaranteed) waulize kwanini hizo buku buku wasiweke wenyewe...