Clouds FM kuwatema watangazaji PJ, Gerald Hando na Abel Onesmo wa Power Breakfast

Hii habari ni upotoshaji. PJ na Hando hawajatemwa ila wamekataa wenyewe kusaini upya mikataba ya ajira sababu wanapunjwa mno mgawo kwa hela wanayoingiza kwenye matangazo.
 
Salaam wana jamvi!

Kuna taarifa yakuwa watangazaji wawili wa Clouds media group,wameondoka kwenye kituo hicho kilichojizolea umaarufu sana kwenye medani ya habari na burudani.

Watangazaji hao walikuwa wana kipindi chao maarufu sana cha asubuhi chenye jina la Power Breakfast(PB)nia ya huu uzi siyo kutaka kuwachambua hawa waliona fursa sehemu nyingine na wakaifuata.

Mashaka yangu ni yakuwa naona harufu ya hii radio kurudi hatua kumi nyuma,sina hakika kama kuna watakaokuja ku-fit kama walivyokuwa hawa wa mwanzo.

Naliona pigo kubwa sana kwa mzee wa fursa Ruge kwa kuondoka hawa wazee wa PB pale clouds media.
 
Yan hapa ndo pa kusoma alama za nyakati kwetu wengine... Ukikuta hamuelewani na boss wako jitumbue mwenyewe usisubir kufedheheshwa
 
A. Chifupa alipita but mambo yalisonga, wapo wengi wabunifu na wenye vipaji tatizo hawajapa nafasi ya kuonyesha jamii walicho nacho, popote akiondoka mtu yupo wa kifiti bila kujali itachukua mda gani..worry out sir
 
Kawaida sana
 
labda kama umeanza kusikiliza hiki kipindi miaka ya juzi, walikuwepo kina masudi kipanya na fina mango walipoondoka watu tulijua huo ndio mwisho wa Pb. lakini walikuja wengine wakafit,
vivyo hivyo katika leo tena alipoondoka amina chifupa wasilizaji wengi walikata tamaa lakini mbona alikuja dina na akafit. clouds ni kubwa kuliko mtangazaji mmoja mmoja
 
Wapo watakao fit,ila wasi wasi wangu ni kwamba isije ikawa kuna wanaojipendekeza kwa boss ili wengne waonekane hawafai au wanahujum kampuni.wasijali kwan kuna redio haitaki mtu kama vijana hawa wana cv safi kabisa na uzoef wa kutosha na maisha ni popote asinyanyasike kisa private job........
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…