Clouds FM warusha kisa cha kushtua!!

Mbona solution vipanga tulishatoa huko nyuma, muwe mnasoma thread.Hakikisha browser yako ina Adobe Flash player utaweza kusikiliza murua.

Adobe Flash player sio suluhisho la kila tatizo la audio streaming, usiahidi mtu kwamba ataweza "kusikiliza murua." Hata mafundi walioandika code ya Windows kwenye site ya Microsoft wanakwambia "...try the following." Kwa sababu huwezi kujua li computer la mtu lina kifaduro gani huko, can't promise jack.

Link ya site haifunguki kabisa, wewe unamhakikishia tatizo ni Flash Player. Wrongo! Hiyo link sio kwamba inafungua the audio streaming automatically, site inabidi ifunguke halafu ubonyeze "play." Hapo ndio flash player inapokuwa executed, kama inahitajika. Kwa hiyo, kwa maelezo aliyokupa, kwamba inaganda kwenye kufungua link, hukutakiwa kuhitimisha kwamba suluhisho ni Flash Player, get it "kipanga" Blueray?

Mwenye tatizo, try this first: Badilisha browser. Kama unatumia, kwa mfano, IE, jaribu Mozilla Firefox, au Flock.
 
Ambao hamjaona.

Poleni sana. Naona hii link kwa sasa hivi imezidiwa kwani wasikilizaji watakuwa wengi saana. Jana nimesikiliza, asubuhi nimesikiliza, ila sasa hivi hata mie inanigomea. Jaribuni kungia baadaye usiku au kujaribu kesho. Naona watakuwa wameweka maelezo mapya na mtandao wao umezidiwa...... Please, try again letter..
 
Nimeona wale wanaolaani watangazaji.

Kama mnataka kuwaasa dada wa kipindi hiki au kuwapa hongera basi wasiliana na mmoja wao ambaye kwenye blog yake kaweka adress yake:-

TUWASILIANE:

mail:dina_marios@yahoo.com
simu:0787 583132
hii ni namba yakipindi 0784 499547

Hii imetoka kwenye BLOG yake :- Dina Marios

Ila msianze kumrushia matusi dada wa watu. Pelekeni tu maoni yenu bila kutoa hasira zenu utadhani ni yeye alibaka ingawa twajua kuwa hana kifaa cha kubakia.
 

Lets deal with this case first......Haya mengine baadae.
Yes, kuna kila ulilosema lakini at this point the issue is Fatuma na rafiki yake. We can raise those other issues when the time is right.....
 

Unapotoa solution hii unakwenda na "ceteris paribus". Huwezi kuanza ku imagine matatizo ambayo hayajaelezwa, ukifanya hivyo what is to stop you thinking kwamba huyu jamaa anajaribu ku browse hiyo website kwa kutumia chungu au sufuria? You can only help with the information provided.

Kabla ya kutoa ushauri huo nilijaribu kufungua site na nikaona site inafunguka, kwa hiyo there is no issue ya kutofunguka kwa hiyo site.Sasa litmus test, au process ya ku narrow down the issue ni yeye mwenye tatizo a install adobe flash player halafu ajaribu tuone.

Sio unakuja na vi criticism bila ya either kujali kutatua tatizo au kuelewa OSI layer na the layered approach to troubleshooting kijana.na kama computer ina kifaduro kingine ambacho hakijaelezwa si tatizo langu kwamba hakijasemwa, na wala halitakuwa tatizo langu kwamba sijakitolea suluhisho, na wala siwezi kusita kutoa solution inayotatua tatizo, kwa kadiri lilivyoelezwa, kwa sababu eti kuna uwezekano wa kifaduro kingine.

Ingekuwa hivyo hata madaktari wasingeweza kutibu malaria, kwa sababu even with blood test results, technically kunaweza kuwa na vifaduro vya aina milioni moja vinavyotoa symptoms zile zile za malaria.

Kama kawaida yako unatoka kwenye issue na kuingiza vi alfu lela ulela, bora hata vingekuwa na mantiki, havina.

Your dry automatons of life devoid stoic wannabe arguments are really weak and totally unconvincing.
 
I believe hii kitu imekuwa over loaded our wanatatizo la kiufundi.
Hope wanalijua hilo.
 
I believe hii kitu imekuwa over loaded our wanatatizo la kiufundi.
Hope wanalijua hilo.

Hawa jamaa pia wana link ila na wao wanadai kuwa Clouds wamezidiwa kwani hawajawahi kuwa na idadi kubwa namna hiyo ya watu kwa muda mfupi. Labda Invisible awaombe hawa jamaa na yeye atuwekee hapa audio.

Baadaye mwaweza kujaribu hapa: PodOmatic Player

au hii hapa : http://hekaheka.podomatic.com/
 
Mlipo Dar na hasa wasililizaji wa Cloudsfm, mmeshapata habari ni kitu gani kinaendelea? Hii Redio naona imezidiwa kiasi kwamba imegoma kabisa kufunguka sasa. Kama kuna mtu amebahatisha kuifungua hii ya tarehe 23/07 basi atujulishe wengine. Jana nimesubiri saa nzima ifunguke, ikagoma ingawa asubihi ilikuwa inafunguka vizuri ila walipoweka hii impya, mhhhh... Sijui wajanza wameiziba hii link?
 

Kuna watu humu hata ukiwaambia kwamba mungu ametusamehe wote na hatutaenda motoni watakurushia matusi na kuelekeza the best way ya kutoa hiyo taarifa mfano upitie kwa katibu kata etc... ...ndivyo tulivyo

Namuunga mkono dina na ge kwasababu hao wanaofuata taratibu wamefanya nini??
 
haya wakuu links now zinafanya kazi naona kulikuwa na tatizo......msibonyeze link hio ya posy kwanza tena maana haifanyi kazi fanyeni hivi...

tumieni link hii Dullonet Tanzania | Just Call it Real Solution for News and Information

alafu nenda kulia chini kuna ki chat room fulan....chini kuna kichwa cha habari cha habari za sauti toka vyanzo mbali mbali...sasa hapo click heka heka toka cloudsFM......zipo za 23 na 24 ile ya 22 haionekani labda itakuwepo baadae
 
Yo Yo,

Nimeingia huko ila nimetoka mweupe. Naona tu maelezo ya Dullo kuwa kila kitu tayari na sioni wapi nionyeze..
 
Yo Yo,

Nimeingia huko ila nimetoka mweupe. Naona tu maelezo ya Dullo kuwa kila kitu tayari na sioni wapi nionyeze..
mkuu pale kwenye chat room chini yake kuna maandishi madogo madogo angalia kuna link ya heka heka...lakini update ni kuwa yule mkware kakamatwa na yuko ndani.....lakini kama mjuavyo bongo kesho atakuwa mtaani......hii ishu ni mie na wewe na kila mmoja wetu kuifatilia maana naona kama ishaanza kufifia....
 
Embu soma hiyo habari hapo chini..inaonekana tatizo hili la watoto kulawitiwa ni tatizo sugu:

Na Martha Fataely, Hai

MKAZI wa kijiji cha Foo, Machame wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro (jina tunalo) anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kunajisi wanafunzi zaidi ya sita wenye umri kati ya miaka 7 hadi 14.

Wanafunzi hao (majina yamehifadhiwa) ni wa Shule ya Msingi Mkwarungo iliyopo wilayani humo.

Taarifa kutoka kwa wazazi wa watoto hao zinasema kuwa matukio hayo yalitokea kwa nyakati tofauti ambapo Julai 20 ndipo waliipata taarifa hiyo.

Wazazi hao ambao walikuwa na hati maalum ya kumkamata mtuhumiwa yenye namba MOS/RB/10064/2009, walisema, watoto wao ameathiriwa vibaya kutokana na matukio hayo.

Aidha, mmoja wa wazazi hao alisema, matukio ya watoto wao kufanyiwa vitendo hivyo yamedumu kwa muda mrefu hadi alipobaini siku hiyo baada ya kumwadhibu mwanawe kutokana na kuwa na tabia ya wizi wa fedha ambazo alidai kumpelekea mtuhumiwa.

"Nilianza kuona tabia ya mwanangu inakuwa mbaya na kiburi kinaongezeka nikaamua kumwadhibu, ndipo alipoamua kunieleza kwamba amekuwa akifanya tendo la ndoa na mtuhumiwa huyo kwa muda mrefu ikiwa ni baada ya kupewa zawadi ya pipi na biskuti," alisema
mzazi huyo.

Alisema, baada ya kupata maelezo hayo alilazimika kumpeleka Hospitali ya Mkoa ya Mawenzi ambapo alipewa kadi namba 257936 yenye namba ya mgonjwa 69-48-08 ya Julai 21 mwaka huu ambapo kadi hiyo ilieleza kuwa mhusika amekuwa akiingiliwa kimwili mara kadhaa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka hospitalini hapo ambapo gazeti hili linayo nakala yake, ilieleza kwamba mmoja wa watoto hao mwenye umri wa miaka 12 amefanyiwa kitendo hicho zaidi ya mara moja huku maungo yake yakionekana tofauti na umri wa mtoto huyo.

Hata hivyo mmoja wa watoto hao ambaye alizungumza na mwandishi wa habari hizi, alieleza kuwa mtuhumiwa alikuwa akiwaingiza ndani kwake yeye pamoja na watoto wenzake.

Alisema, wenzake wa kike walikuwa wanne na wa kiume wawili ambapo alikuwa akifanya nao kitendo hicho, pia alisema kuwa wengine aliokuwa akiingia nao chumbani humo anawafahamu kwa sura lakini hajui majina yao yote.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mawenzi, Bw. Wilbrod Saganda, alikiri kupokea idadi kubwa ya wanafunzi Julai 21 ambao walionesha kunajisiwa.

"Hapa tunapokea wanafunzi wengi ambao huingiliwa kimwili na watu wakubwa, wanafunzi hao ni mingoni mwao, kwa taarifa zaidi wasiliana na Jeshi la Polisi utazipata kwa undani kwani ugonjwa ni siri ya mtu, lakini wale wanamamlaka," alisema Bw. Saganda.

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Bw. Lucas Nghoboko alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo, alisema hana taarifa lakini aliahidi kufuatilia.

source : IPP Media. 24.07.09
 

Inasikitisha sana lakini hiyo ndiyo picha halisi ya mambo.Na tukio kama hili ndio kimekuwa chazo cha watu kujichukulia sheria.Fikiria angelikuwa mtoto wako-wengi mungelikuwa mumeisha maliza kazi huyo mohamedi yuko ahera.
Uongozi hakuna kabisa.Kungelikuwa na uongozi waziri au IGP personally angelienda kumshika huyo kijana kuonyesha uongozi wao.
 
Mwawado,

Hii ni too much sasa. Serikali ni kama haipo na watu wanajichukulia madaraka mikononi kwa kila kitu. Watu wana uhakika wa kufanya kitu na mkono wa sheria usiwaguse.

Unategemea nini Waziri wa mambo ya ndani anapokuwa Masha? Viongozi wa chama na serikali wenyewe hawaheshimiki na wamejaa Ufisadi na ufuska tu. Watu wanapata habari jinsi viongozi wao wanavyotesa na vimwana na hata wake za watu (Marehemu Ditopile), acha wanafunzi wa secondary hadi University.

Sasa wale wajinga wa mitaani wao ndiyo wanakwenda chini kabisa kuchukua vitoto vidogo. Kama sheria zingelikuwa kali, basi wenyewe wangeipata habari yao. Pana wakati hadi naona labda Tanzania baadhi ya sheria za Kiislaama (sharia) na kukata mikono, kuuwa nk ziingizwe kwenye katiba na zianze kufanya kazi.

Ningeliweza, basi hawa watu ningelianzisha biashara ya viungo vya binadamu. Kabla hatujamuuwa, basi tunachukua kila kinachohitajika kama macho, moyo, maini, figo, damu nk na kuziuza kwa wanohitaji na pesa hizo zinapewa kuwasaidia watoto waliokuwa affected na mijinga hii. Mkimaliza kungoa basi mnamuuwa.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…