1. Mikataba ya migodi ni mibovu - Kweli inahitaji kazi, lakini kwanza tuielewe ili tusirudie makosa, pili tuhakikishe tuna capacity ya kuregulate hii sekta na kushiriki kikamilifu.
2. Tunapata ONLY 3% from revenue ya madini - Wrong, 3% ni value ya extraction na siyo revenue. Vile vile kuna njia nyingi za ku-track revenue inayobaki nchini siyo kodi na royalty pekee!
3. Migodi imetililisha sumu katika mito kama Tighitte na watu pamoja na mifugo imekufa- Mpaka leo hamna vipimo vilivyoweza kuthibitisha madai ya vifo vya binadamu wala mifugo. Hizi habari za kupashana mtaani tuziacheni watanzania...No Research, No Right to Speak!. Wewe inkuingia akilini maiti za watu 44 na mifugo 700, amabao wote wamekufa ndani ya wiki 3 eti hazionekani? waliodai kuzika hawataki kuonyesha makaburi! Hii mipasho kuna siku itafanya watanzania wapigane kwa mambo ambayo hayapo.
4. Watu waliwahi miminiwa risasi na walinzi wa migodi na wengine waliuwawa na hamna aliekamatwa kwa kuua. Porojo nyingine hizi hapa - Once again folks u have to do ur reseach, walinzi wa makapuni (haswa extractive industry) ambayo yako listed kwenye NYSE hawatumii silaha za moto, kutokana na makampuni hayo kuwa signatories waVoluntary Principles on Security & Human Rights. Kwa hivyo hawa mabwana wanatumia virungu, tear gas na 'rubber bullets'. wanaomimina hizo risasi ni FFU...acha projo!
Leo hii PJ na Power Breakfast, niseme Cluods FM wamesimama na kufagilia migodi ya walanguzi. Hii ni haki? Si ni usaliti huu? Mimi ninampongeza PJ kwa kuwa na ujasiri we kwenda kujionea mwenyewe. Wengi wetu hapa tunajishibisha na material za internet na baadhi ya magazeti lakini hatuja kaa na kujaribu kufanya utafiti wa kina.
The range of what we THINK and DO is limited by what we fail to notice. And because we fail to notice that we FAIL to notice, there is little we can do to change; until we notice HOW failing to notice shapes our thoughts and deeds. Otherwise we will waste time pondering solutions for a unrelated problem. That is the risk we run by ranting without understanding the issue.
PJ, unadhani hatujui kwamba ulikaribishwa na wana Barrick, ukalipiwa malazi na ukapandishwa ndege yao, unategemea sisi tutaamini kwamba utawaponda? Hao jamaa wanafanya PR ili tuwaone niwasafi na wanatusaidia. Hamna kitu. Ni capitalist wanataka kupata faida lukuki ya madini na watimke baadae na kutuachia mashimo. Mimi na wewe PJ tutabaki hapa hapa TZ. Hiyo cheap PR unawapa haitafautiani na ile ya Richmond kuweka matangazo katika magazeti na kudai ni kampuni halali. Nani aliamini? Wapo watu wenye upeo mdogo wakuchambua mambo wakaamini. Na wewe unatakata tukuamini? Mimi nitoe!
Ukasema tena kwamba eti hatuwezi kuiendesha migodi sababu gari moja inayobeba mchanga wa madini linaizwa $1,000,000. Tujilize, walieba hela kupitia Kagoda waliiba liasi gani? Tsh. 40billion. Hizo hela zinaweza nunua migari haina hiyo mingapi? Na Liyumba je?
Anashutumiwa kuiba Tsh. 220billion, nae angenunua migari mingapi? Sasa nikuulize PJ, hao jamaa zako wa Barrick, hizo investment wanatoa mifukoni mwao au wanakopa? Sisi hatuwezi kukopa au kuiba BOT tuka invest katika migodi yetu? Kaka hizo investment PJ alikuwa anazungumzia ungeenda kujionea kwanza. Mining is the most capital intensive sekta, high risk alafu long term returns...ni balaa. Mgodi wa underground kama ule wa Kahama unahitaji $900 million kujenga, bado haujaingiza hesabu za exploration ambazo huwa haziwi recovered. Hapo huanzi kuzalisha mpaka baada ya miaka 2. Alafu baada ya shughuli kuanza you have to do capital re-investment ili kuweza kuendesha mgodi, bado haujazungumzia umeme, barabara, maji, wafanyakazi...sikukatishi tamaa lakini naomba ukasome kidogo kabla hauja-propose mambo ambayo hayaeleweki!
Huu ni ujinga watu kama PJ na watawala wengine wanataka tuamini kwamba hatuna uwezo wakuchimba madini yetu. Nakataa.
Ombi langu kwako PJ na wana Clouds wenzako nikwamba, waTZ waleo sio mbumbumbu. Tunaelewa. Tunachambua na tunatafari. Huwezi tupumbaza kamwe.
Sekta ya madini Tanzania inayo matatizo mengi lakini siyo hayo ulioyataja hapo juu. Kumbuka kwamba unapozungumzia hii sekta serikali yako ilijiwekea malengo kwenye Vision 2025; ikasemaa kwa kufungua sekta ya large scale mining inatarijia ifikapo 2025, sekta hiyo itachangia asilimia isiyopungua 10% ya GDP - pato la taifa. Leo hii sekta hiyo inayumba ikichangia kati ya asilimia 2.4 mpaka 3! Lakini wakati huo huo ndiyo sekta inayokuwa kwa kasi kuliko sekta nyingine zote, including telecoms. Sasa hapo jiulize, how is that possible? The 'simple answer' ni kwamba serikali imekosa mikakati maalum ya kuhakikisha kwamba sekta inakuwa na fwd and bwd linkages to the economy. Vile vile ukiangalia nchi ambazi zimetutangulia kwenye biashara hii utagundua wamevuna mapesa mengi zaidi kutokana na supply chain za migodi. Ndizo zilizopanua tax base, kuibua employment oppurtunities na kuwezesha kukua kwa middle class. Tusidanganyike na ongezeko la royalty na kodi, kwani hizi no siasa tupu. Mrahaba na kodi siyo sustainable, kwani zinakuwa limited na uwezo na performance wa hiyo sekta.
As they say, nothing is complete and thus nothing is exempt from criticism.