Clouds FM yafagilia Walanguzi?

Huyo anayeitwa PJ anastahili lawama kama anavyostahili lawama Mkuu wa mkoa wa Mara, RPO Mara, Mkuu wa Wilaya Tarime/Rorya na OCD. Wako wengine ambao kwa taarifa nilizonazo wako kwenye payroll ya Barrick.

Bahati mbaya Barrick ki-historia hawajawahi kuwa wazuri. Jaribu ku-google kampuni ya Barrick na mazingira. Sehemu kubwa ni lawama za mabaya yake. Bahati mbaya zaidi kwetu TZ ni mazingira pamoja na corruption!

Spika Six alipokuja juu kumunyamazisha Mb. Cheyo, pia ilisikika kwamba kapata kitu ili Barrick isijadiliwe kwa ubaya. Yaweza kuwa kweli maana sikumbuki kusikia taarifa ya Kamati ya Bunge juu ya North Mara ktk kikao kilichopita kama ilivyoahidiwa. Hata hivyo sitegemei la ajabu maana hata NEMC waliishia kutoa matamko ya kisiasa pamoja na nguvu ya kisheria waliyo nayo.

Kama NEMC ilishindwa kusema mambo ya kitaalamu, itakuwa kamati ya Bunge? Kamati nyingi za Bunge hazina uwezo wa kitaalamu kiasi cha kuichunguza North Mara.

Nasema haya ili kuonyesha kwamba, Barrick imewateka wengi ktk nchi hii. Kila mtu analipwa kwa kiwango chake kulingana na nguvu yake ktk serikali. PJ yeye anaweza kuwa ameishia kupewa pesa ya lunch na kupanda ndege lakini iko siku utaambiwa TZ tulikuwa tunapewa sehemu ndogo ya kipato cha madini kwa sababu sehemu kubwa ilikuwa ikiwekwa akaunti ya Rais kama ilivyokuwa Zaire ya Mobutu au Ilikuwa ikichukuliwa na chama Tawala.
 

hata mimi pia hapa nimeshindwa kuvumilia, hivi mtu kufanya uchambuzi mpaka awe na cv? What are we trying to create here. Do you mean to say those who dont have a good education background cannot make sound decision and analysis?

Hebu tuwaangalie hao maprofesor wetu, mbona basi hawawezi hata kutengeneza calculator. Sisi watz tunaojiita wasomi what have we contributed in the world of technology? Mimi naona huu ni ulimbukeni wa elimu, ni kama vile kipofu aliyeona ngamia kisha akarudi kuwa kipofu, kila kitu atakifananisha na ngamia. Mtu akisema kitu basi ni tupe cv yake. This is not right. Wewe unayetaka cv za watu what have you achieved from the education you have got. Am talking about tangible achievement. If you want to criticize a point, do it constructively.
 
Nafikiri ni kazi sana kunyoshea vidole mtu mmoja mmoja katika mfumo wa kibepari ambao ndio umeshaota mizizi hapa kwetu. PJ ni part ya huo mfumo and so is clouds. Clouds are part ya huo mfumo and they also can be used to serve its interests. Msemo wa wahenga nafikir unasema 'mjumbe hauwawi'. Pj katumika kama chombo kusafisha uoza wa Barick, ni kama alivyo Tewel pia, sema PJ yupo katika chombo cha habari. Tujiulize je PJ ni mtu anafuata mrengo gani wa kifikra na kuuamini, angekua sio mbepari angeamua kukaa kimya asipande kwenye kipindi aachishwe kazi akale majani..Lets deal na mfumo huu wa manyanyaso- au tuurekebishe - at least to a social democratic system- kama inaezekana, upuuzi wa Barrick unaweza kushugulikiwa serious zaidi.
 
Biashara siyo kupotosha umma.Chombo cha habari ni pamoja na maakama, bunge na serikali ni mihimili mwingine ya dola.unapoongelea dola ni chombo cha umma.chukulia bunge au maakama waanze kupotosha umma tutawachukuliaje. Angalia sheria za kusadili vyombo vya habari hakuna kipengele hicho unachosema cha kupotosha umma ilimradi unapata faida.chunga sana unapochangia.
 
Ni dalili ya kwamba watu wanaelewa ukweli na kwamba hawataki kupotoshwa au kudanganywa.
 
Bahati mbaya Barrick ki-historia hawajawahi kuwa wazuri. Jaribu ku-google kampuni ya Barrick na mazingira. Sehemu kubwa ni lawama za mabaya yake. Bahati mbaya zaidi kwetu TZ ni mazingira pamoja na corruption!

Dow Jones Sustainability Index ranks Barrick as world leader

Barrick Gold Corporation (NYSE:ABX) (TSX:ABX) has been named to the Dow Jones Sustainability World Index (DJSI), ranking the company as a top performer in corporate social responsibility worldwide for the second consecutive year. Barrick was first listed on the prestigious DJSI World index in 2008, and has been part of the North America listing since 2007. The renewed listing on both indices reinforces Barrick's position among the most sustainability-driven companies in the world.


The DJSI World tracks the performance of 2,500 leading companies worldwide. Launched in 1999, the index independently evaluates long-term economic, environmental, and social performance using objective benchmarks to identify the top 10% of performers in areas of sustainability. Kwa taarifa zaidi kuhusu DJSI, visit www.sustainability-indexes.com

Watanzania tucheze na facts, tuachane na porojo. Ni kweli ukitembelea web site kama www.protestbarrick.net kuna mambo mengi kuhusu hii kampuni lakini kwenye dunia ya leo kuna wanaharakati wenye agenda zao, pia kuna wanamazingira wanaopinga aina fulani za sekya na wapo wanaotafuta mbinu endelevu za sekta bila ya kuumiza mazingira.
 
Nadhani watu wanashutumu bila kuwa na data.....someni utafiti wa dr .semboja ndo mtajua nani ni nani kwenye madini..

Katika kila wakia moja inayouzwa kutoka kwenye migodi, serikali inapata jumla ya kodi mbalimbali ya asilimia 15 , production cost ni asilimia 61, kulipa madeni ya benki asilimia 12, faida kwa mwenye mgodi asilimia 10, community services 2

sasa hapo wizi uko wapi? Tatizo lipo kwenye matumizi ya hizo asilimia 15 inazo pata serikali wanazitumia je? Mathalani watu wanataka mwekezaji awaendeleze jamii inayozunguka migodi, je serikali inafanya nini? Je kila mwenye biashara anafanya hivyo....

Mfano mzuri ni royal kingdom of mafikeng south africa, wao wanapata royalty asilimia 3 ya kila mgodi ulio kwenye aridhi yao, kwakuwa viongozi wao wanajali wananchi wao, wamewajengea nyumba wananchi wao wote, wanawasomeshea watoto na pia wanawekeza kwenye sekta nyingine ili mali ikiisha wasitaabike....wamejenga uwanja kwa ajili ya world cup 2010 pale rusternburg...
Tuangalie akili za watanzania, sasa
wilaya ya kahama walilipwa milioni 220 kama mgao wao kutoka bulyankulu, milioni 110 walilipana malimbikizo ya posho za vikao, milioni 50 walitumia kwenye vikao vya kamati mbalimbali

tarime wao walitumia fedha zao zote (milioni 220) kulipia wanafunzi wa sekondari.....kwa mfano huo tu utaona tatizo ni sisiem na viongozi wao hawana vipaumbele, wao ni chama chao, wao wenyewe wananchi baadaye
 

Mimi ndicho nilichosema, naona hata kuwaita lowbrow ni kuwa elevate, they are ridiculously gross.
 

Ghana wametangaza juzi hapa wanatumia USD 10 bn kujenga nyumba bora 200, 000.

Nyumba bora 200,000 for goodness' sake. Na sisi ndio tunashikilia nafasi ya tatu kwa uzalishaji wa dhahabu Afrika baada ya South Afrika na Ghana.

Lakini sie hatuoni chochote cha maana, hata kusema tufanye kitu angalau cha thamani ya a tenth of what Ghana is poised to do.

Hakina kuna vi Mobutu na vi Abacha vinajificha serikalini.
 
Wakuu tukumbuke kwamba inasound so cheap kuattack personality badala ya hoja. Pili who said mtizamo wako ndiyo standard ya mitizamo ya wengine? Na kwamba yeyote anayefikiri otherwise basi hajui, ni msaliti, fisadi etc.?

Ok tuje kwenye hoja. Uchimbaji madini na biashara yake ni so complex kuliko watu wanavyofikiria. We always miss a point tunapodiscuss suala hili nayo ni facts.

Kwa mfano mleta thread anazungumzia bei ya dhahabu kutoka $300 mpaka $1200. Anasahau kwamba mafuta at tht time yalikuwa kama sh 500 kwa lita, umeme je? mishahara at that time ilikuwaje? Bei ya chuma (Nyenzo muhimu kwa spare parts) ilikuwaje?

Pili kuna hili lakusema kama Equipment ya mining inauzwa $1,000,000 basi tungetumia hela za kagoda na liyumba then we would be mining on our own. What a joke? Ingekuwa hivyo basi hizi Barrick, Rio Tinto, Anglo, BHP zisingekuwepo Australia maana they are a rich nation and can buy all the equipment required na pia wana utaalam wa mambo ya madini. Canada pia, US etc. This is the same kusema kwamba ukiwa na hela ya kununua mabasi 200 basi you can buy them and be beat all the bus owners in TZ. Pia tukumbuke mabenki hayakopeshi or will do so with huge interests kama huna utaalam na uzoefu biashara unayotaka kufanya.

Sisi bao tulipigwa kwenye mikataba. Mfano instead of 3% mrahaba ya faida tungeweza kusema 5% of ounces produced tunachukua uwe umeingia hasara au faida. Pili tungeweza kusema bidhaa zote za mgodi ziagizwe na makampuni ya kitanzania. I am sure lots of people will b skeptical about this. Lakini what happens as of now ni kwamba bidhaa nyingi za madini kutoka marekani, ulaya na Australia zina mamiddleman wa kisauzi. i.e Kitu kinazalishwa marekani lakini kinakuwa ordered from South Africa, kinaenda SA ndipo kinakuja Tz. Tungeweza pia kusema supply ya maji na umeme ifanywe na wafanyabiashara watanzania serikali ikiwadhamini. Hili nalo linaweza kuonekana gumu lakini kuna mifano Maji ya Mbeya cement na Mbeya Textile yanakuwa supplied na kampuni za wananchi. Cha msingi ni kuwa na reservoir say a dam.

Masuala kama ajira na career development za watanzania yalitakiwa yachambuliwe kwa kina kwenye mikataba. Instead of just a vague sentencekwamba tutatoa ajira na mafunzo.

Naamini kama tuna nia na serikali yetu ikawa na nia bado hatujachelewa. We can start from where we are tukajifunza makosa tuliyofanya, tukabuild a true and fair partnership na wawekezaji. Pia ikumbukwe wawekezaji hawavutiwi tu na absence/low of taxes na amani na utulivu. Ni mchanganyiko wa mambo mengi kuondoa bureaucracy serikalini, cheap and reliable Utilities (electricity, water etc) Good infrastructure (roads,railways, ports etc) competent workforce etc.
 
Kulogwa ninakozungumzia mimi hapo ni ''literary''. Nadhani umenielewa sasa!

Mhhh ... kulogwa unakokuongelea ni literary? you cant be serious! NO wonder unawatetea Barick pamoja na uharamia wote walioufanya dhidi ya wananchi wa North Mara.
 

Yaani watu wanatengeneza mabilioni ya faida kutokana na dhahabu ya watanzania na wao wanatoa dola laki mbili tu? laki mbili tu? na wewe sifa zote unamwaga!


Kuna mtu aliwahi kuniambia kuwa wakati wakoloni wanaingia afrika (kina karl peters), walikuwa wanawapatia mababu zetu peremende, vikoi, na vizawadi vya kishenzi (kama ugoro) na wanasainishwa mikataba kibao ya ardhi.

Inaonekana Masaki ungekuwepo enzi hizo, ungeuza hadi wanao ili upewe peremende. Yaani Barick wamejenga soko unaloliita la kisasa (lina gharimu kiasi gani?) na wewe meno yote nje bila kuona kuwa hii ni peremende tu unapewa ili ukae kimya wakati wao wakijichukulia wanavyotaka.


No mkuu, tatizo la kwanza hapa ni wawekezaji. Wao wanabeba lawama kwa kila kinachotokea kwenye biashara zao.
 
That argument is completely irrelevant here. Ulitaka Barrick waiambie serikali kwamba hapana jamani, 3% ni kidogo sana, tunataka kulipa 20%? Ungekuwa wewe ndiye mwanahisa mkuu wa Barrick ungefanya hivyo?

Ndio, ningekuwa mimi ni mwanahisa wa Barick ningefanya hivyo. Ningekataa kuruhusu kampuni kufanya unyonyaji wa hali hii kwa watu masikini.



Masaki,

watu wasio na hatia wanapigwa risasi muda mwingi tu bongo na sehemu mbalimbali duniani. Umesahau kesi ya Zombe? Unakumbuka vifo vya Kombe, Mkemia mkuu wa serikali etc wakati ule?

hao watu wanaofuata sheria za nchi so far sio barick ambao walikwenda kusaini mkataba wa buzwagi hotelini na waziri wa serikali ya Kikwete.



Amedhalilishwa, period. Hoja ingejengwa kwamba hana utaalamu wa kujua kiasi dhahabu inayochukuliwa, si kwamba eti alipewa chakula, malazi na kupandishwa ndege ya Barrick ili apotoshe ukweli. Huko ni kudhalilisha!

Ni ukweli kuwa alipewa yote hayo?

PJ amejidhalilisha mwenyewe na sio vinginevyo

Tatizo leni mkishakaa sana nje ya nchi basi mnadhani kila mtu anajua misamiati ya USA.....House Negro(!?) Ndio nini?

U- house negro ni kile unachofanya hapa ... kutetea slave master (wanyonyaji wa Barick) wako kwa kudhani kuwa wewe ni bora zaidi ya watumwa wengine (wananchi wa north mara wanaokufa kwa sumu za barick).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…