Bibititi1
JF-Expert Member
- Sep 28, 2014
- 464
- 218
Wapendwa habari za masiku leo napenda tupitie huu uzi mdogo hapa wenye kufurahisha nimeutoa mahali.....
Bila mawazo ya Dj Jooh kusaga labda Clouds Fm isingekuwepo hapa ilipo mara nyingi tunakutana sehemu za Starehe na kuongea mambo ya maisha ya kila siku na ya kawaida kabisa! Ilikuwa ni tofauti kwa Dj Kusaga na rafiki yake kipenzi Ruge Mutahaba siku zote walifikiri tofauti wakati Dj kusaga akipiga ngoma kali na Ruge akicheza mziki kwa madaha hisia zake zikampelekea kuwaza huenda siku moja huu mziki ninao ucheza hapa naweza nikaumanage na watanzania wakapata kilicho bora zaidi. Haya ndiyo yalikuwa mawazo ya Dj Jooh mziki ambao naupiga mashabiki wanaucheza huenda siku moja nikapata nafasi ya kuujengea heshima. Mawazo haya akayatimiliza kutoka kwenye dhahania kwenda kwenye mawazo halisi. hakusita kumueleza wazo hili rafiki yake Ruge Mutahaba na akalipokea kwa mikono miwili, kwenye maisha ni safari ndefu iliyojaa miiba na mbigiri pamoja na kukatishwa tamaa siku zote waliamini wanaweza kwa kuheshimu na kuthamini mawazo yao ila kila walipokwenda kupeleka mawazo haya walikwamishwa na katu hawakukatishwa tamaa lakini hawakusita kutimiliza ndoto yao hatimaye mwaka 1994 ndoto hii ilitimia Clouds Fm ikaanza kupiga mziki rasmi na kuwa kituo cha burudani kwa vijana nchini .....
Somewhere in Arusha wakati Clouds FM inapasua anga alikuwepo kijana mdogo umri wa miaka 5, David Omary aliyependa kusikiliza na kucheza muziki japokuwa alikuwa mdogo Mama alikiona kipaji chake mwanae alipenda kuzungusha sahani kila anapokula na kupiga kelele alikwisha leta hasara nyingi za kuvunja sahani za udongo mpaka akaanza kupewa chakula kwenye sahani ya bati, Ndoto za kijana huyu zilichanua na mwangaza ulikuja baada kijana David Omary kufika Mwaka wa kwanza Chuo kikuu ndipo alipokutana na Dj maarufu bongo aliyekuwa na kituo cha Mafunzo ya Udj huyu si mwengine ni Dj PQ Mara ya kwanza ilikuwa ngumu sana kuaminika kutokana na muonekano wake wenye haiba ya upole kama ilivyo kwa muonekano wa Boss Joseph kusaga, kamwe usilinganishe muonekano na Karama aliyonayo mtu ndani yake unaambiwa kwa kimombo Never understimate The power of Someone Untill U try him or her, yaani usiidharau nguvu ya mtu kabla hujawahi kumjaribu. kijana huyu alipata nafasi na kuwa miongoni mwa vijana wazuri wenye kujua kuchanganya muziki huku akisoma na kupiga muziki kituo cha Radio fulani.
Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds media Group ndugu Ruge Mutahaba aliweza kusikia ladha ya uwezo wa miaka 20 nyuma aliyokuwa akiipata kipindi anakwenda kucheza mziki mzuri uliokuwa ukipigwa kwa ustadi na uliochanganywa vyema na Dj Jooh kusaga.....! hapa ndipo scout team ilipoagizwa kuingia kazini kumsaka David Omary popote alipo aje kunogesha ladha ya mjengoni akisaidiana na wakali kama Dj Zero, Dj Steve B, Dj Bullah, Dj Too short, Dj Fetty, Dj Mully B, Dj Elly mzee wa Night Kali na wengine kibao wakongwe kama Dj Peter Moe, hatimaye scout team ilifanikiwa kumnasa kijana huyu kinda machachari na kumuingiza mjengoni. hapa ndipo dunia ilipofunguliwa kwa Daudi Omary mabibi na Mabwana niruhusu nimtambulishe kwenu "Kutoka kwenye mikono yenye kasi ujazo na nguvu huyu ni Mr Washawasha Dj D Ommy ...................... Leo hii ni miaka 17 ya Clouds FM ndoto ya Dj Joseph Kusaga pamoja na Ndugu Ruge Mutahaba kusimamisha kituo bora cha radio kwa burudani na habari namba moja Tanzania na Afrika na mafanikio pomoni kituo hichi iliyoyapata tangu kuanzishwa kwake zinachagizwa na Tuzo mbili kubwa barani Africa kwa Dj D Ommy kama Best Dj In Africa akiwamwaga Madj wote wakali Afrika wenye majina na Ukongwe kwenye hii tasnia kwa kushinda Tuzo ya AEAUSA na AFRIMMA wana mwali wamekwisha wasili kuna kila sababu ya kusherekea na kujivunia vya kwetu ni Faraja kwa Clouds FM we are super brand kazi zetu zikipenya mbali zaidi... this Friday Tuzo zote zinatua mjengoni tega sikio kwa kishindo cha November 5 ...... Imooooo!