Clouds FM...

Wadau niko mkoa wa mara naomba kujua frequency za cloud fm ni ngapi? please
 
Wanao ipata Clouds Kwa Moro wanipe frequency tafadhali
 
Radio 1 ni radio kubwa? Sema ilikuwa kubwa, saiv bongo radio kubwa ni moja tu.
 
TCRA anasimamia frequency za Ving'amuzi, Mitandao ya simu, TV na Redio
Hayo masafa hununuliwa pale unapokuwa na vigezo vya kurusha sehemu hizo ulizoomba, Pia watu hununua masafa kwa malengo ya baadae,
Kuna redio moja mwanza 94.1, ya Msama, alinunua masafa muda sana ila hakuwa hewani baadae ndio akaanzisha kituo, walioanzisha nyuma yake walipewa 102.5, 100.4 kina Lake na Mkombozi.
Hata Dialo hununua masafa na kureseve ili wengine wakipewa wawe mbali na masafa ya kituo chake kuhakikisha usikivu hauingiliani na redio zingine,
Mfano, Redio One 102.7 na Lake fm 102.5 kwa Mwanza kuna muda huingiliana.
Sijui nimekujibu..?
 
Huwa wananunua bei gani frequency kwa mkoa mmoja?
Nina ndoto badae nikitulia nianzishe online radio nianze roughly na budget kiasi gani?
 
Ndo nilikuwa sijajua hili kumbe mpaka utegeshe sehemu ndo utaiskia moja kumbe zinaingiliana
 
Wasafi wa juzi wamepataje 88.9 au kusaga alinunua Masada zamani
 
Visit website ya TCRA kuna kila kitu mpaka jinsi ya kupata leseni
Hebu nisaidie, hivi minara ya radio hutofautiana? Mfano radio one,radio free afrika usikivu wake mkubwa sana hata sauti ni nzuri,je radio nyingine za FM usikivu ni duni hata nguvu ya kitambo haba nisaidie ukubwa wa mitambi km wtts au kv nahitaji nijue hayo.
 
Hebu nisaidie gharama za matangazo kwenye radio au TV zikoje? Mfano matangazo ya live ya TV au radio gharama ikoje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…