Clouds, Mama ana Nyota yake, imetosha

Clouds, Mama ana Nyota yake, imetosha

lulu za uru

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2015
Posts
2,557
Reaction score
3,221
Nawasilimu kwa jina la Jamuhuri ya Muungano wa Tz.naona clouds wameanzisha promo ya praise and worship kwa mama.

Ni hivi huyu mama hahitaji promo imetokea tu watu wengi kumpenda kama nyota za kina mama zilivyo amekuwa na charisma ya kupendwa hii promo mngeitumia hata kupinga vitendo vya ukatili wa watoto mama angewahi sana kuwapigia hiyo simu mnayoisubiria kwa hamu....

Dahuu, Geah Na Jose Mara katika kipindi chao cha Leo tena huwa wana segment ya hekaheka hu-report matukio mbalimbali ikiwemo ukatili wa kingono kwa watoto Geah Habibu mkuu wa Segment hiyo anasema hapo huwa haripoti vitendo vyote vya kikatili kwa watoto kubakwa, kulawitiwa kutokana na muda wa hekaheka kuwa mdogo yaani ni Vingi mno.

Mitaani watoto wana mengi wakuu ukisikiliza masikio mpaka yanawasha kama una MTT utalia kabisa hao walawiti na wabakaji wengi wakipelekwa vituoni kesho wanadunda mtaani..kwnn hiyo movement ya kupinga hii kitu wasitumie platform hiyo? Hebu angalieni jamani au ndio ile mwenye nacho huongezewa?

Mungu anawaona.
 
Wahuni hawa inabidi wafokewe kama vile wapo enzi za Shujaa. Wameshiriki kuitafuna nchi enzi za dikteta asiyehojiwa
 
Kuna watu wanakosa muda mpaka kusikiliza hizi fm radios 📻, daaah aisee.....
 
Hawajaanza leo ni wazee wa fursa. Enzi za Jk walikuwa wanamfanyia mpaka birthday kabisa.
 
Hivi babykabae wa clouds 360 yupo wap????
 
Back
Top Bottom