Clouds Media imepoteza mvuto

Clouds Media imepoteza mvuto

Hziyech22

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2019
Posts
15,351
Reaction score
21,362
Naona kabisa moja Kati ya redio iliokuwa na power Sana kwenye enteinment Ni hii.Ukiangalia miaka ya nyuma ukipita nyumba 7 basi Kati ya hizo 5 utakuta zinasikiliza clouds fm ila kwasasa hiv Hali ya imebadilika clouds imepata ushindani mkubwa kutoka Wasafi media na Efm ila hasa hasa Ni Wasafi media ambayo imepata audience wengi Sana.

Sababu kuu ya kupoteza mvuto Ni pamoja na clouds kumpoteza Ruge.Ruge aliwa Ni mbunifu Sana na genius kwenye hii tansinia na pia alikuwa ana connection na Serikali na ushawishi mkubwa pengo lake pale Ni kubwa ambalo sizani Kama litazibika tena.

Athari zimeanza kuonekana ukiwemo Fiesta iliyofanyika bila Ruge kupoteza mvuto na mtu ambaye alikuwa royal Sana kwa Ruge Bdozen kusepa na vipindi vingi vya clouds kuanza kupoteza mvuto ikiwemo Xxl Sasa hiv Xxl imegeuka kuwa Kama kijiwe Cha kahawa uoni leader wa kipindi Kama alivyokuwa Bdozen.

Kipindi Cha shilawadu kimekufa, Leo Tena tangu wamweke Mwijaku kimepoteza mvuto na anachangia kiasi kikubwa kukiharibu.Kipindi ambacho nakiona kimebaki kinaibeba clouds Ni Cha Millard Ayo.
 
Back
Top Bottom