Clouds Media ni media ya kinafiki sana

Magnesium

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2014
Posts
317
Reaction score
185
Habari wanabodi.. Leo nimeona niandike hili.

Nieleweke kabisa mimi sina timu yeyote hapa.. Hivi majuzi tulishuhudia clouds Media kujitangaza kuwa bila wao diamond asingefika pale na wanajivunia kwa hilo.. Baada ya muda akarud Ali Kiba na jinsi walivyompromote kupitia vituo vyake vya redio na televisheni tunaona ni wazi kabisa wana lengo la kuendeleza na kichochea bifu baina ya Ali kiba na Diamond.. Hayo yote yakapita ila hili la juzi limezidi, promo aliyopata na anayopata mpaka sasa Ali Kiba kupitia tour yake ya #ChekechaCHEKETOUR ni kuegemea upande mmoja kwa kumpa promo kupitia matangazo na hata post mitandaoni..

Imefika mahali wamempa hadi mtangazaji wao Mussa Hussein (mwanadaresalam) kuzunguka nae kwenye hiyo tour... Ukiangalia jana Diamond alikuwa na performance kubwa kwenye tuzo kubwa kimataifa nchini Nigeria lakini hakupata support yeyote kutoka kwenye hii Media.. Ndio maana nasema ni wanafiki kwa kuwa lengo lao sio kuongeza ushindani bali ni kukuza bifu...
 
Kweli kabisa na nilishasema hata hawa wasanii hawajielewi kwa upande mmj au mwngne
 
ze pipo stesheni bana badala ya kumpa promo nas b nas maujanja, wanampa promo star aliyetoka tayari na bifu juu!
 
Mi' nishaacha hata kusikiliza wala kuangalia chochote kupitia clouds media, wa ovyo sana wale
 
chuki binafsi haifai eeh,"in alichoki voice"
 
Mbona kila siku mnawaongelea hawa tu??
 
ze pipo stesheni bana badala ya kumpa promo nas b nas maujanja, wanampa promo star aliyetoka tayari na bifu juu!

ata mimi huwa siwaelewagi hawa jamaa inaonekana wananufaika sana na mabifu kila siku wao tu? sasa huo ni usengerema! watu wawil wanapopigana kisha kumshika mtu mmoja na kumuacha mwingine!
 

Na nyie mnaowaongelea wasanii wawili ni wanafiki sana, wasanii wapo wengi mbona msiwaongelee?
 
Na nyie mnaowaongelea wasanii wawili ni wanafiki sana, wasanii wapo wengi mbona msiwaongelee?

Tunawaongelea na wengine wengi tu lakini penye ukweli tutasema hata kama tutakuwa tunawaongelea kila siku wale wale.. N of course hawa ndo Icons wa Muziki Tz lazima kuwaongelea..hawaepikiki
 
ata mimi huwa siwaelewagi hawa jamaa inaonekana wananufaika sana na mabifu kila siku wao tu? sasa huo ni usengerema! watu wawil wanapopigana kisha kumshika mtu mmoja na kumuacha mwingine!

Yap nimekusoma..true that.. Haiwezekani wapigane watu wawili half umshike mmoja mikono
 
Clouds wanataka msanii wanayempangia nini cha kumlipa ila sio msanii wa kuwapangia nini wamlipe. Wanataka msanii anayewasujudia ili waweze kumyonya vinzuri kwenye malipo. Ukiangalia ishu ya Alikiba, anapigiwa promo sana kwa sababu wao Clouds wanajua kupitia tour zake watatengeneza pesa, ila Alikiba watamlipa kiduchu. Wanafanya hivyo kwa sababu wanajua kwa sasa Alikiba anahangaika kurudi kwenye chati kama ilivyokuwa zamani hivyo chochote watakachompangia kumlipa atakubali tu.

Kwa upande wa Diamond wameshaona hawamuwezi, hawana tena uwezo wa kumpekesha kama ilivyokuwa zamani. Leo hii Diamond focus yake ni kimataifa ambako haitaji msaada wa Clouds kuweza kufika huko. Ni bahati mbaya kwamba Clouds wana tabia ya chuki za kijinga ambazo si nzuri katika ukuaji wa sanaa ya muziki hapa bongo. Kwa level aliyopo Diamond sasa hivi ilipaswa ingekuwa changamoto kwao Clouds kuweza kuwapa moyo wasanii ambao bado hawajajulikana kimataifa ili waweze kufikia level hizo.
 
PA ya Kiba imelipiwa ndo maana unaona inatangazwa vya kutosha. Tuzo za Mond zinabaki kuwa kama sehemu ya habari ya chombo husika kwani ni habari za burudani kama habari zinginezo. Ndio maana zinakua na muda mchache. Zipo Band nyingi mfano wa Malaika Band au FM Academia kila wiki zinafanya ziara na kufanya show mbalimbali kwenye makumbi bshaka mnasikiaga zikitangazwa pale studio, ukilipia laki 300000 show yako wanaitengenezea tangazo na kuipromote.

Tour ya Kiba kalipa hela nyingi kidogo ndio maana imepewa nafasi kubwa inatangazwa karibia kila kipindi. Hii hata Weusi washaifanya Mwishoni wa mwaka jana hadi wakambeba dj zero na b12 Kwenye ziara yao na wasanii wengineo kibao tu wanafanya(ga). Mbona hujagi kutoa mapovu? Ni kama tangazo la kibiashara la Tigo na makampuni mengine makubwa. Mbona hujiulizi kuanzia Power Breakfast, leo tena, xxl,jahazi na amplifaya unakuta kampuni moja inapatikana karibia vipindi vyote vya siku? Ina maana wadhamini wengine walalamike kwa upendeleo? Hahahahahaha...ujinga mzigo. Kadri unavyomwaga hela ndivyo unapewa airtime ya kufamtu.

Au mlidhani hii kanuni ina aply kwa makampuni tu na sio wasanii? Au mnadhani wasanii hawafanyi biashara ya kazi zao?
Kuna muda wa kutangaza kazi za wasanii kama sehemu ya vipindi lakini vilevile kuna muda special unalipia unapewa promo kulingana na bei yako.

Habari za Diamond wanatangaza kama media nyingine zinavyomtangaza. Mbona hujiulizi huko kulikoni? Ndio maana hata Diamond mwenyewe hawezi kuja kulalamikia huu upuuzi wako. Mambo mengine wanayajua watu wa industry husika ndio maana hayawapi shida.

Msiwe mnakurupuka kutoa lawama kama hamjui mambo yanavyoenda. Uliza upewe ufafanuzi, usipolidhika ndo utoe lawama zako.
 

mi nnachojua clouds hawawez kumpa promo kiba bila kutoa mkwanja au makubaliano yao wote wapo kibiashara akimpa promo kiba bure je kampuni inaingiza nn so hela ndo kila kitu lipa upate promo.
 

Good... Unafahamu ya kwenye Industry.. Lakini una uhakika Ali Kiba kalipa hiyo pesa unayodai? Wakati anatoa wimbo wa Mwana pia alilipa promo? Siku ya show ya Fiesta kwa hy Alikiba ndo alilipa sio wao kumlipa? Ni kweli kabisa unachosema lakini tofautisha pesa wanayotoa wadhamini wa vipindi au segment kwenye kipindi na wasanii kupata promo.. Huu ni ukweli usiopingika kwamba Clouds wanakamata fursa, wakiona hela watapiga tu hela.. Ukitaka umaarufu usiokuwa na tija wanyenyekee.. Kwa promo anayopata Ali Kiba ni zaidi hata ya hayo makampuni maana katawala hadi mitandao ya kijamii... Videos na picha za show kila time... Sikatai kutoa support kwa wasanii hasa wanaofanya vizuri ila wao wanatumia chance ya bifu lao wao kuwa upande wa Ali Kiba..
 
ata mimi huwa siwaelewagi hawa jamaa inaonekana wananufaika sana na mabifu kila siku wao tu? sasa huo ni usengerema! watu wawil wanapopigana kisha kumshika mtu mmoja na kumuacha mwingine!

Ngoja siku wapigane ndo watu wataamini kwamba hawa jamaa haziivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…