Clouds wanavyosota kumwangusha Hanstone

Auto-Marvelt

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2019
Posts
1,653
Reaction score
3,336
Miongoni mwa upcoming starz wanaofanya poa kwenye gemu la mziki wa bongofleva in msanii 'Hanstone'. Kijana anafanya poa sana kama walivyo kina Marioo, Mbosso Khan, Whozu na wengine kama buku ila huyu kijana wee weka mbali na watoto.

Kijana huyo jina lake ni Hassan Ramadhani Masanja mtoto wa aliyekuwa gwiji wa mziki wa kitanzania marehemu Banza Stone aliyetamba kwa vigoma kama Elimu ya mjinga, Supu ya kuku wa kienyeji na mtaji wa maskini anasema atamkumbuka baba yake sana kwani alikuwa mstari wa nyuma kwenye mziki licha ya kumshauri aachane na mziki ajikite kwenye Elimu

IPO HIVI, baada ya mzazi wake kutangulia mbele za haki, kijana huyo mwenye umri wa miaka 19 aliamua kumuenzi kupitia mziki na alianza kuonekana kupitia kibao cha iokote alichoshirikishwa na msanii Maua Sama.

Hata mtoto mdogo anaweza kukuambia Hanstone in nani kupitia ngoma hiyo. Baadae kijana Hugo aliamua kutoa ngoma yake mwenyewe 'acha lipite' akaja na 'i miss you mama' ngoma bora kuwahi kutokra kwenye historia ya bongo fleva.

Radio Mawingu waliweza kumpa support ya kufa raia hadi akatamba bongo mwishoni mwa mwaka jana na mwaka huu mwanzoni 2018/2019 lakini saivi mambo yanaanza kwenda kombo.

WCB WAHUSIKAAA.

Inasemekana kwamba miongoni mwa sababu kuu za kuzimwa na radio Mawingu basi Wasafi media inahusika kutokana na uhasama uliopo haina ya Mawingu na WCB.

Baada ya Hanstone kuonekana pamoja na CEO wa WCB Diamond platnumz na baadhi ya mamaeneja wake ikadaiwa kwamba msanii Huyo anaweza akasajiliwa na Wasafi hivyo Mawingu wakaanza kumuweka kando.

CHIBONGE YAHUSIKAA
Baada ya kijana Hugo kutoa kollabo Kali pamoja na Marioo ya Chibonge basi clouds wakakataa kuipa promo hapo nyimbo yenyewe kwa kuwa ni kali ikajipa promo yenyewe.

Ili kumzima Hanstone, Mawingu walikuja na mpango wa remix ambayo ilishirikisha Marioo, Abbah na G. Nako ambayobimepewa nafasi za juu sana kwenye chart yao ya top 20 lakini kiuharisia ngoma hiyo haijaifikia ile ya awali hata nusu.

Wale wanaojua kusoma nyakati naamini mtanielewa, kwa leo niishie hapo
 
Mkuu nilianza kukuamini ila ikabidi nishuke uliposema Chibonge Remix ni kazi ya Clouds FM! Pitia baadhi ya intavyuu za Hanscana na Abbah (waliokua mameneja wa Hanstone kabla hajazingua) halafu uje ufute huu uzi
 
Wanajaribu kuzima nyota ya bwamdogo lakini hawataweza, mtoto ana talanta ya hali ya juu mno! nadhani dabliusibii wameona potential yake, wakimsaini watakuwa wamelamba dume!
 
Dah wabongo bwana lazima watafute wakumtwisha zigo. Aliyebeba zigo la lawama muda wote RIP Ruge toka atangulie mbele ya haki naona bado masuala ya lawama yapo.
Nilitegemea sasa wasanii waache kulalamika wapige ela maana waliyedai anawanyonya keshafariki
 
Unajua sababu yao ya kumtema mkuu
Mkuu nilianza kukuamini ila ikabidi nishuke uliposema Chibonge Remix ni kazi ya Clouds FM! Pitia baadhi ya intavyuu za Hanscana na Abbah (waliokua mameneja wa Hanstone kabla hajazingua) halafu uje ufute huu uzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…