Club African vs Young Africans: Players performance Rating - Yanga

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
4,016
Reaction score
6,759
Hii ni summary ya ufanisi wa wachezaji wa Yanga katika mechi ya jana. Alana ni katika fractions za /10 . Ni mawazo huru ambayo yanaweza kupingwa na kukosolewa Kwani watazamaji hatufanani. Karibu tuchambue!

- Diarra 9
Huyu golikipa anaweza kuwa ndiye nyota ya mchezo kwa siku ya jana. Aliitika vyema pale ilipohitajika. Uzoefu wake ulimfanya aweze kumudu vyema presha za ugenini kwa waarabu. Alicheza Mashuti kadhaa langoni kwake pamoja na mipira ya 50/50 lakini alikuwa ni beki ndani ya kipa kwa kuongeza umiliki wa mipira wa Yanga. Dakika za mwishoni alicheza mipira mingi sana ya kutenga. Aliipanga vyema defense yake.

- K.Shomari 7
Licha ya kimo chake alijitahidi sana kukabiliana na mashambulizi ya kustukiza toka kwa waarabu. Tatizo pekee alilokuwa nalo ni kupandisha timu na umiliki wa mpira. Ni katika mabeki punda waliotimiza vyema majukumu yao ya upunda akisaidiwa na Moloko. Kutokupanda mbele hovyo kulisaidia kujenda balance kati ya kushambulia na kuzuia kwa timu.

- Lomalosa 6
Jana alibadilika sana ktk kujenga uwiano wa kupanda na kushuka. Alijenga idadi ya watu nyuma na kuweza kupunguza makali ya mpinzani. Jioni alianza kuchoka, kufanya makosa mawili na upande wake ukaelemewa hasa kutokana na BM33 kutomsaidia sana kukaba. Tangu kufika jangwani jana ndo ameoverperfom. Akitunza ubora ule atakuwa na msaada huko mbele.

- Y.Bengala/D.Job 8.5
Wamepiga kazi Si ya kitoto jana katika partnership ya hali ya juu. Yannick alileta uzoefu wake halisi ukichanganya na kasi na kipaji cha Job eneo Lao ndo lilikuwa eneo bora kwa timu ya Yanga usiku wa jana. Interceptions na cut-out zilikuwa za kutosha kwa Pacha hii.

- Khalid Aucho 8
Amerekebisha kwa kiasi kikubwa udhaifu wake kuchelewa kukaba timu inaponyanganywa mpira. Alikuwa na utulivu mkubwa na alijitahidi kuhold possession kwenye Zone yake kwa pasi za uhakika. Kadi ya njano ilimpunguza Makali , alichoka na kuumia mara kadhaa kutokana na wapinzani kujaribu kumuondolea utulivu. Anahitaji kuongeza kasi katika kufukuza mpira(upunda)

- Jesus Moloko 6
Credits kubwa kwake ni kujituma sana na kumsaidia Kibwana kucontain presha ya wapinzani katika ukabaji. Kasi yake ilimfanya awe live mchezoni akiendana na kasi ya mpira. Utulivu katika ‘Final third’ lilikuwa tatizo lake na kushindwa kulink na Fiston.

- B.Morrison 7.5
Jana aliweka utoto pembeni na aliamua kufanya kazi. Licha ya uvivu wake lakin Alishuka mara kadhaa kuchukua mpira na kujaribu kuondoka nayo single-handedly . BM33 alikuwa ndo mwiba katika SAFU ya ulinzi ya wapinzani akitengeneza Faulo nyingi sana. Kuna wakati alikuwa anapoteza mipira kizembe sana. Walimfahamu kwa utukutu wake na walijaribu kumtoa mchezoni mara kadhaa lakini alijitahidi kuwa makini sana. Performance yake kubwa sana tangu msimu uanze ni jana.

- Sure Boy 8
Midfield Maestro wa jana, alimpunguzia mzigo Aucho pale kati kuliko Double Pivot iliyokuwa na Feisal Kwani ni mwepesi kwenye kukaba kuliko Fei.Wepesi ,ufupi na kasi yake ya kubadili uelekeo ulisaidia Yanga kumiliki Duara na kusumbua viungo wapinzani wenye miili. Alikuwa anajaribu kumchezesha Mayele kutokea katikati ya uwanja kwa Tap-in kadhaa. Last attempt ikazaa Goli !!

- Aziz Ki/ Farid Mussa 7 (Super Subs)
Hawakucheza muda mrefu lakini ni kama vile walikuja kuamua hatma ya mechi. Farid Aliongeza ubora kwenye mapungufu ya Moloko katika kumiliki mpira na kushambulia. Aziz Ki alileta ‘Class’ nyuma ya Fiston, jambo ambalo Feisal lilimshinda. Wangeanza baada ya Half time yawezekana ubao ungekuwa 0-2 .

- Feisal Salum 6
Alishindwa kutimiza majukumu yake kama Namba 10 . Hali hii inamkutaga hasa katika game ambazo wapinzani wanatumia Nguvu na Akili kwa pamoja. Hili lilisababisha kupotea kwa Fiston. Aliporudi katikati alianza kusumbuliwa na tatizo la kukaba. Ubora mkubwa aliounesha ni kusaidia umiliki wa mpira eneo la kati. Kwa uwezo wake tunaoufahamu anaendelea kuwa Flop tena kwenye mechi za kimataifa.

- Fiston Mayele 6.5
Hakuwa yule tunayemjua vyema, waarabu walimdhibiti vyema. Hakusogelewa sana na viungo wake wa ushambuliaji. Kama ilivyo ada anaweza kukupa kitu bila kutegemea katika mazingira yeyote. Pasi ya kichwa kwa Aziz Ki imezaa goli. Hili limemuongezea point kadhaa na kusamehe kupotea kwake licha ya kurudi mchezoni dakika za mwishoni baada ya Goli. Bado anabaki kuwa mchezaji Muhimu katika mechi kubwa.

- Bakari Mwamnyeto 5
Hakuwa na muda wa kutosha, lakini alipoingia aliongeza Namba kwenye eneo la 18 la Yanga , na alihusika katika kuokoa mipira kadhaa. Nyakati hizo waarabu walikuwa wanapiga mipira mirefu, Ni Mwamnyeto alikuwa anahitajika kukamilisha ulinzi wa Yanga. Alitimiza jukumu hilo kwa 90%
 
Hivi huyu siyo Ally Kamwe kweli!
 
Sipingi.
Ila kwangu namuona Sure boy ndio kila kitu jana.
 
Upo vizuri......Nategemea popoma gentamycine ajifunze kwako
 
Uchambuzi uko njema sana huu.
 
Yanga kwakweli ligi ikiisha wakae chini watulize kichwa walete majembe ya ukweli waache usajili wa mara kacheza Newcastle mara sijui wapi,kule afrika magharibi kuna wachezaji kibao kuliko hawa mizigo kama tuisila,bigirimana,makambo,kambole,moloko.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…