Babalevo ni mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mtangazaji wa
Wasafi FM, Mchekeshaji na Balozi wa makampuni mbalimbali. Zaidi ya kuwa kwenye tasnia ya burudani Babalevo amewahi kuwa kiongozi wa kisiasa (
Diwani) wa Kata ya Mwanga, Manispaa ya Kigoma Ujiji kupitia Chama Cha
ACT Wazalendo
Babalevo kama mfanyakazi wa Redio ya Wasafi FM husikika akizungumza mambo mbalimbali ya kijamii, kiasa na kimichezo katika kipindi cha jioni kinachoitwa Jana na Leo kinachoanza saa 11:00 jioni mpaka saa 2:00 usiku.
Leo Desemba 4, 2024 katika Mtandao wa X (Zamani Twitter) imeibuka chapisho lenye nembo ya Wasafi Media (litazame
hapa) likiwa limemnukuu Babalevo akisema kuwa "Watu wenye akili ndani ya
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (
CHADEMA) hawazidi kumi".
Upi uhalisia wa Post hiyo?
JamiiCheck imefuatilia chapisho hilo kupitia Google Reverse Image Search na kubaini chapisho hilo lililoibuka leo lilichapishwa mara ya kwanza kwenye Mtandao wa X (
hapa) Septemba 24, 2024 na kusambaa zaidi Septemba 25 na 26, 2024 (tazama
hapa na
hapa). Sehemu zote Post hii inasambaa ikiwa picha tu na nukuu hiyo lakini hakuna Video ikimuonesha Babalevo akitamka maneno hayo kuhusu
CHADEMA
Zaidi ya hayo, Ufuatiliaji wa Kimtandao uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa post yenye maneno hayo na nembo ya
Wasafi Media haikuwahi kuchapishwa katika kurasa zao rasmi za Mitandao ya kijamii na wala haikuwahi kuwekwa kwenye Akaunti rasmi za
Babalevo.
Uchambuzi wa Posti husika
Uchambuzi wa JamiiCheck umebaini aina ya Mwandiko (font type) iliyotumika katika post hiyo iliyomnukuu
Babalevo haifanani na font wanayoitimia
Wasafi Media katika kuchapisha Taarifa zao nyingine.
Aidha, Uchunguzi wetu kupitia Akauni ya
Babalevo umebaini kuwa Siku ya Septemba 21, 2024 msanii huyo alionekana akisafiri kuelekea Dubai (Tazama
hapa) ambapo mpaka siku ya September 24 ambayo post hiyo inatoka
Babalevo alikuwa bado Dubai na hakuwa Redioni (Tazama
hapa).
Hivyo, kutokana na ufuatiliaji huu tumejiridhisha kuwa Taarifa hii imetengenezwa na haina uhusiano wowote na Babalevo na Wasafi Media.