PostGE2025 CNN: Polisi walitumia Silaha za Moto kuua waandamanaji

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Heparin

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2021
Posts
450
Reaction score
3,368


Uchunguzi huru uliofanywa na CNN kufuatia mauaji ya Oktoba 29, 2025 umebaini Mamlaka za Tanzania kupitia Jeshi la Polisi zilitumia nguvu kubwa kudhibiti waandamanaji, kiasi cha kusababisha mamia ya watu wapoteze maisha.

Katika uchunguzi wake, imebainika pia baadhi ya miili ya watu waliouawa wamezikwa kwenye makaburi ya Pamoja kwenye Makaburi ya Kondo.

Hii inathibitishwa na picha za Satelite za kabla na baada ya Oktoba 29, pamoja na makundi mawili ya watetezi wa haki za binadamu.

Pia soma CNN: Video za Mochwari za Sekou Toure Mwanza na Mwananyamala DSM zenye miili ya waandamanaji waliouawa ni halisi

Chanzo: CNN
 
Kwa hiyo ni picha za satellite au ushuhuda wa mtetezi wa haki za binadam unaoonesha maelfu wamezikwa kwa kondo?
 
Kwa hiyo ni picha za satellite au ushuhuda wa mtetezi wa haki za binadam unaoonesha maelfu wamezikwa kwa kondo?
Pole kwa kukupa kazi ngumu ya kusafisha uovu uliofanyika, kaa kwa kutulia usubiri muda ukupe majibu.
 
Hivi kama kuna location imeoneshwa na CNN kwamba inahisiwa kuwa na makaburi ya halaiki raia anashindwa nini huko waliko kwenda kufukua?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…