CNN yamfukuza kazi mtangazaji kwa kumsaidia kaka yake mwanasiasa

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
Mtangazaji wa Marekani Chris Cuomo amefukuzwa kazi na CNN baada ya kumsaidia kaka yake, gavana wa zamani wa New York Andrew Cuomo, alipokuwa akipambana na madai ya unyanyasaji.

Uamuzi huo ulikuja baada ya CNN kusema kuwa habari za ziada zimeibuka juu ya kiwango cha ushiriki wa Chris Cuomo katika utetezi wa kaka yake mkubwa.

Andrew Cuomo alijiuzulu mnamo Agosti baada ya waendesha mashtaka kusema alikuwa amewanyanyasa wafanyakazi.

Chris Cuomo, mwenye umri wa miaka 51, amesema katika taarifa kwamba amekatishwa tamaa na "sio jinsi ninavyotaka wakati wangu kwenye CNN umalizike".

Alifanya kazi kwenye mtandao huo tangu 2013 na akawa mmoja wa watangazaji wake wa habari wanaotambulika, hivi karibuni akiongoza matangazo ya CNN ya uchaguzi wa rais wa 2020 wa Marekani.

Taarifa ya CNN ilisema kwamba "kampuni ya sheria inayoheshimika" iliajiriwa kuchunguza juhudi za Chris Cuomo kumsaidia kaka yake mwanasiasa kupambana na madai ya unyanyasaji wa kijinsia.

Lakini wakati mchakato huo ulivyofanyika, "taarifa mpya imefichuka" na kusababisha mtandao huo kusitisha mkataba wake mara moja".

Chris Cuomo alikuwa tayari amesimamishwa kazi na CNN siku ya Jumanne baada ya kufichuliwa kwa juhudi zake za nyuma ya pazia za kusaidia kusafisha kashfa hiyo.

Wakati huo, mtandao huo ulisema kwamba ingawa "unathamini nafasi ya kipekee [Chris Cuomo] aliyokuwa nayo na kuelewa hitaji lake la kuweka familia kwanza na kazi ya pili", ushauri aliotoa kwa kaka yake ulikuwa ukiukaji wa maadili ya uandishi wa habari.

Hati zilizotolewa na Mwanasheria Mkuu wa New York Letitia James siku ya Jumatatu zilionesha kwamba Cuomo mdogo aliendelea kushinikiza wafanyikazi wa gavana kumruhusu kuchukua jukumu kubwa katika utetezi wa kaka yake.

"Unahitaji kuniamini," alituma ujumbe mfupi kwa Melissa DeRosa, katibu wa kaka yake, mwezi Machi, na kuongeza: "Tunafanya makosa ambayo hatuwezi kumudu."

Pia aliahidi kuwasiliana na vyombo vingine vya habari vya Marekani ili kujaribu na kujua kuhusu madai mengine ambayo yalikuwa yanakuja.

Katika barua pepe ya wafanyakazi , ambayo New York Times iliiona, Rais wa CNN Jeff Zucker alisema: "Inaenda bila kusema kwamba maamuzi haya sio rahisi, na kuna mambo mengi magumu yanayohusika."

Kufukuzwa kwa nyota huyo kutaibua maswali mazito kuhusu viwango vya uandishi wa habari nchini Marekani.

Mwandishi wa habari wa CNN Brian Stelter alisema kuwa "watazamaji wanahitaji kuwa na uwezo wa kuamini kile wanachosikia hapa kwenye runinga tunapoangazia taarifa nyeti, hata ikiwa inahusisha mwanafamilia wa mfanyakazi mwenzako".

Familia ya Cuomo kwa muda mrefu imekuwa moja ya wadau wakubwa katika siasa za Marekani.

Andrew Cuomo alichaguliwa kwa awamu tatu mfululizo kama gavana wa New York na baba yao Mario aliongoza jimbo hilo kwa zaidi ya muongo mmoja kati ya 1983 na 1994.

Kabla ya kujiuzulu mnamo Oktoba, Andrew Cuomo alikuwa kiongozi mkuu wa kisiasa, kabla ya uchunguzi uliofanywa na Mwanasheria Mkuu wake kuhitimisha kuwa alikuwa amewanyanyasa kingono na kuwapapasa wanawake 11 wanaomfanyia kazi.

Chanzo: BBC Swahili
 
Damu nzito kuliko maji. Style hiyo ingekua bongo hata kwa wapambe tu ingekua balaaaa
 
Oh too bad,nilikuwa nampenda sana chris cuomo

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Huku kwetu mtu anamsaidia ndugu yake kwenye uchaguzi ashinde
 
Mambo ya CNN na madai ya unyanyasaji yanatuhusu nini sisi? Wao wanajadili huu mgao wetu wa umeme? Kila mtu ashinde match zake.
 
🙄🙄 Habari mchanganyiko.
 
🙄🙄 Habari mchanganyiko.

Mchanganyiko wa mambo yenye tija kwetu hata wao hawafuatilii mambo yasiyo na tija kwao. Nenda CNN uone kama wanamuongelea Mbowe au mgao wa maji TZ.
 
Huenda wanafanya hivyo sababu hawana idhaa ya Kiswahili.
Ila kama wangekuwa na idhaa ya Kiswahili ni kawaida kukuta Habari kama hizo.
 
Back
Top Bottom