Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Klabu ya Coastal Union imethibitisha kuvunja mkataba na aliyekuwa mlinda mlango wao, Ley Ngumbi Matamp ambaye alikuwa golikipa bora wa msimu wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara msimu uliopita kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Taarifa ya leo Desemba 10, 2024 ya leo kupitia ukurasa rasmi wa klabu hiyo iliyoambatana na picha ya nyanda huyo raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesema:- "Tunakutakia kheri nyingi na mafanikio zaidi katika maisha yako."
"Tumefikia makubaliano baina ya klabu yetu na golikipa wetu Ley Ngumbi Matamp ya kumaliza huduma za pande zote mbili. Uzoefu wako umechangia kwa asilimia kubwa mafanikio yetu ya msimu uliopita" imesema taarifa hiyo.
Matampi alijiunga na Coastal Union msimu uliopita 2023/2024 akiwa mchezaji huru baada ya kumalizana na FC Lupopo ya Congo, na msimu huo aliibuka kuwa kipa bora wa msimu.