Coastal Union yahama Uwanja wao wa nyumbani Mkwakwani

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
22,719
Reaction score
40,739
Uongozi wa klabu ya Coastal union umewajulisha rasmi mashabiki na wadau kwamba timu hiyo itautumia Uwanja wa Sheikh Amri Abedi, Arusha kama uwanja wake wa nyumbani kwa michezo yake inayofuata.

Taarifa iliyotolewa na ‘Wanamangush’ leo Oktoba 10, 2024 imebainisha kuwa uamuzi wa kupeleka mechi Jijini Arusha umezingatia mambo mengi sana yakiwemo kuthamini pendekezo la wanachama na wapenzi wa klabu hiyo.

Mambo mengine yaliyozingatiwa ni kuibakisha timu katika Kanda ya kaskazini, kuthamini kazi kubwa anayofanya mkuu wa Mkoa wa Arusha ya kuinyanua Kanda ya kaskazini kupitia Jiji la Arusha, ombi la muda mrefu la Wana Arusha na uhakika wa kupata alama 3.

“Tunawaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuendelea kuipa sapoti timu yetu nguvu na ari ile ile. Hata sasa kazi kwenu Wana Arusha timu Bora kutoka ukanda wenu hiyo.” imesema Coastal Union
 
Timu kama Coastal Union yenye historia kubwa na Tanga haitakiwi kuhama kiholela hivyo. Hapo wameshaelewa kujenga uwanja mkubwa Arusha bila kuwa na timu ligi kuu ni kosa kubwa kwa hiyo wanajaribu kufunika kosa lililofanyika. Uwanja ungejengwa Mbeya, Mwanza au Morogoro wala wasingehitaji kufanya yote haya.
 
Timu kama Coastal Union yenye historia kubwa na Tanga haitakiwi kuhama kiholela hivyo. Hapo wameshaelewa kujenga uwanja mkubwa Arusha bila kuwa na timu ligi kuu ni kosa kubwa kwa hiyo wanajaribu kufunika kosa lililofanyika. Uwanja ungejengwa Mbeya au Morogoro wala wasingehitaji kufanya yote haya.
Akili kama hizi ndio Mangungu anazipenda
 
Timu kama Coastal Union yenye historia kubwa na Tanga haitakiwi kuhama kiholela hivyo. Hapo wameshaelewa kujenga uwanja mkubwa Arusha bila kuwa na timu ligi kuu ni kosa kubwa kwa hiyo wanajaribu kufunika kosa lililofanyika. Uwanja ungejengwa Mbeya au Morogoro wala wasingehitaji kufanya yote haya.
Mbeya wanaitenga sana hawa wanasiasa
 
Karibuni sana Costal Union Arusha.

Machalii ya R wanawakaribisha kwa moyo mkunjufu.

Ushindi ni lazima.
 
Uongozi wa klabu ya Coastal union umewajulisha rasmi mashabiki na wadau kwamba timu hiyo itautumia Uwanja wa Sheikh Amri Abedi, Arusha kama uwanja wake wa nyumbani kwa michezo yake inayofuata.

Taarifa iliyotolewa na ‘Wanamangush’ leo Oktoba 10, 2024 imebainisha kuwa uamuzi wa kupeleka mechi Jijini Arusha umezingatia mambo mengi sana yakiwemo kuthamini pendekezo la wanachama na wapenzi wa klabu hiyo.

Mambo mengine yaliyozingatiwa ni kuibakisha timu katika Kanda ya kaskazini, kuthamini kazi kubwa anayofanya mkuu wa Mkoa wa Arusha ya kuinyanua Kanda ya kaskazini kupitia Jiji la Arusha, ombi la muda mrefu la Wana Arusha na uhakika wa kupata alama 3.

“Tunawaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuendelea kuipa sapoti timu yetu nguvu na ari ile ile. Hata sasa kazi kwenu Wana Arusha timu Bora kutoka ukanda wenu hiyo.” imesema Coastal Union
Uwanja wa Mkwakwani una shida gani au ukarabati bado unaendelea?
 
Back
Top Bottom