Coastal yajivunia Alikiba

elivina shambuni

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2018
Posts
461
Reaction score
295
BAADA ya kurejea tena katika Ligi Kuu Tanzania Bara, Coastal Union ya jijini Tanga imejipanga kufanya vizuri katika msimu ujao wa ligi hiyo ambayo inatarajiwa kuanzia Agosti 22, mwaka huu, huku ikiweka matumaini makubwa kwa mshambuliaji wao, msanii Alli Kiba.

Akizungumza na gazeti hili jana, Kocha Mkuu wa Coastal Union, Juma Mgunda alisema anajivunia wachezaji aliowasajili katika msimu huu ambao mmoja wao ni msanii maarufu wa Bongo Flava nchini, Kiba, kuwa wamejiandaa kupambana kuhakikisha wanatwaa ubingwa.

Mgunda alisema kikosi chake kina wachezaji wengi vijana ambao wana nguvu na uwezo wa kupambana na wapinzani huku akiongeza kuwa hakuna timu wanayoihofia.

Kocha na mchezaji huyo wa zamani wa Coastal Union, alisema pia wamejipanga kucheza mechi nyingine za kirafiki tatu kabla ya kuanza kwa ligi ili kutoa nafasi kwa kila mchezaji kuonyesha alipofikia na kupata kikosi cha kwanza ambacho ni imara.

"Tunaendelea vizuri na mazoezi, nina matumaini makubwa sana na vijana wangu, hata hao waliosajili wachezaji wazee najua nao walianzia katika ujana, uzoefu haununuliwi, wana morali ya hali ya juu na wako tayari kupambana katika vita ya Ligi Kuu, " alisema kocha huyo.

Aliongeza kuwa Coastal Union imejipanga upya na itaanza msimu mpya kwa nguvu kuhakikisha haipotezi pointi katika mechi za awali kwa sababu haitaki kurejea ilikotoka na kujiweka kwenye hatari ya kushuka daraja kila wakati.

Mbali na Coastal Union, timu nyingine zilizopanda daraja ni pamoja na JKT Tanzania, African Lyon, KMC FC zote za Dar es Salaam, Alliance FC (Mwanza) na Biashara United ya Musoma mkoani Mara.
 
Ali Kiba atakuwa pale kibiashara zaidi. Wajanja tunajua sana haya mambo.
 
Wakati Simba wako na diamond platnumz kama brand ambassador wao, Kiba yeye hana makuu kaamua kujiunga na coastal kabisa,kweli huyu jamaa hapendi show off!
 
Toka enzi za kina Mohamedi Salim,Yahaya Dondwe,Said Jack,Hemed Morocco,..

Siku zinaenda kasi sana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…