Coco Beach kulikoni, kumepita kimbunga au yanafanyika maandalizi ya kupaboresha?

petrol

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
626
Reaction score
455
Asubuhi hii nimepita barabara ya baharini nikielekea Sea Cliff Hotel. Pale maeneo ya Coco Beach ambayo ni maarufu kwa mihogo ya kukaanga nimeona vibanda vyote vimebomolewa isipokuwa msikiti.

Kumepita kimbunga au yanafanyika maandalizi ya kuboresha eneo hili maarufu?
 
Ukiona hivyo jua pameshauzwa kimya kimya maana sijasikia taarifa yoyote rasmi kutoka mamlaka inayohusika. Why wamebomoa kimya kimya
 
Mkuu Rais alitoa pesa vibanda vijengwe vya kisasa zaidi na maboresho ndio wafanyabiashara warudi.
 
Sasa mbona umepita bila picha au ni kambi ya Jeshi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…