CHA The GREAT
JF-Expert Member
- Nov 11, 2010
- 651
- 854
COINTELPRO ni nini?
Ilikuwa program maalumu ya siri na wakati fulani haramu, ndani ya shirika la kijasusi la ndani la Amerika, FBI, kati ya mwaka 1956 hadi 1971. Program hiyo, ililenga kudhibiti chama cha kikomunisti nchini humo, Socialist Party-USA, taasisi za kisiasa na viongozi wa taasisi hizo (hasa za watu weusi), wanaharakati na wote waliopinga vita ya Vietnam.
Waliolengwa na mpango huo ni pamoja na mwanaharakati Martin Luther King Jr., na Black Panther Party. Kadhalika waliolengwa na program ya COINTELPRO, ni pamoja na kundi la 'Republic of New Afrika' kusini mwa nchin hiyo, kundi lililotaka kujitenga 'secession' kwa watu weusi kusini mwa Amerika.
Kundi hilo lililengwa na mpango huo kutokana na kile kilichoitwa vitendo vya ubaguzi wa rangi 'racism' pamoja na kuunga mkono kwa kikundi hicho kutaka kuundwa kwa Jamhuri Mpya ya Afrika--'Republic of New Afrika'
Njia zilizotumika na program hiyo, ili kufanikisha malengo yao, zilikuwa ni kusakizia watu kesi (Planting) kama vile kuficha dawa za kulevya kwenye makazi ya watu ili ionekane watu hao wanajihusisha na biashara ya dawa za kulevya, kuweka na kuficha mabomu ama silaha kwenye makazi ya watu ili watu hao waonekane na kuhusishwa na ugaidi.
Vyombo vya sheria kama vile mahakama navyo vilitumika vibaya kwa kushirikiana na shirika la FBI, ambapo ushahidi wa uongo ili kuwatia hatiani watu ulitolewa mbele ya vyombo vya sheria, wakati fulani mauji, na inaaminika FBI ndiyo waliomuua Martin Luther King Jr., kama sehemu ya program hiyo--COINTELPRO.
Program ya COINTELPRO ilikuwa ya siri mpaka mwaka 1971, ambapo tume ya raia wa Amerika kuichunguza FBI ( Citizens' Commission to Investigate the FBI) ilipoingia kwenye ofisi kuu za FBI na kuchukua nyaraka mbalimbali ambapo ilikuja kubainika kuwa vitendo vingi vilivyotekelezwa na mpango huo vilikiuka haki za kiraia na kuvunja katiba ya nchi hiyo.
Na katika sehemu ya report ya tume hiyo, ilisemwa kwamba, watu au hata taasisi mbalimbali za kisiasa zilizolengwa (targeted) na program hiyo, hazikujihusisha na vitendo vya kigaidi na wala havikuwa tishio (subversive) kwa Amerika.
Program hiyo ilikomeshwa mwaka 1971, na Mkurugenzi wa FBI wa wakati huo, J. Edgar Hoover, ndiye aliyehusika kwa kiasi kikubwa kuratibu na kutoa maelekezo ya nini cha kufanya katika utekelezaji wa program hiyo.