COL.MAHFUDHI: Zanzibari and Tanzanian internationalist


When people run of ideas...wanatumia mabavu kuendelea kuwepo.
 
Kuna ukweli mwingi nyuma ya mapinduzi unafichwa,kwa faida ya wanasiasa wachovu na waoga wanaoogopa vivuli vyao.Tunajua kuwa aliye taka sana kutumiwa njia ya fujo ni Babu.Huyu mkomunisti ndiye alianzisha mpango wa kupokonya madaraka kwa kuwatumia vjana waliotoka cuba na urusi.Karume alipendelea zaidi Mazungumzo zaidi.Babu alipendelea fujo zaidi na aliamini ndio njia pekee ya kumtoa sultani(rejea hotuba ya babu ya siku ya uhuru 1963).Hata historia ya Tanganyika nayo inapotoshwa makusudi ili kujustfy mambo waliyo fanya kinyume.Ndipo namuelewa mzanganyika anaposema juu ya usaliti..(rejea sababu za samul doh kuchukua madaraka)
 
sasa huyo polisi aliyetoa silaha,Edington kisasi aliishia wapi? NA je huyu somebody HANGA je did he play any part katika haya mapinduzi?
Ndg kwanza la kufahamu ni kuwa,okello alijipenyeza zanzibar baada ya maumau na "kumalizana"na kenyata.Alifanikiwa kuingia hata kuwa police kwenye serikali ya sultan.Kilicho saidia mapinduzi ni kutimuliwa kazi kwa askari polisi wengi akiwemo okelo.Askari wapya hawakuwa na uzoefu wa kutosha wa mapambano.
 
"kuna kipindi kimoja kilikuwa kinaendeshwa na mmarekani mmoja mweusi kilionyeshwa jamaa alikwenda nchini Kenya sehemu za coastal region na alifanya mahojiano flani na jamaa wa swahili na walijinasibu kuwa wao sio waafrika walijinasibu kuwa wao ni wairani."

Alikuwa ni Professor Henry Louis Gates Jr., wa Harvard University. Aliwahoji akiwa Tanzania mwaka 1999 katika documentary series yake, "Wonders of the African World," PBS. Alipowaambia mbona ni weusi kama yeye, walimjibu wao siyo Waafrika ni Wairani.

Miaka mingi kabla ya hapo, alikuja Tanzania 1969, akiwa mwanafunzi (first-year student) Yale University. Alifanya kazi kwa mwaka mmoja hospitalini, Kilimatinde, na madaktari na manesi kutoka Australia ambao alisema walikuwa ni wabaguzi sana na dharau sana kwa Waafrika, watu weusi. Alipokuja tena Tanzania, alisema Tanzania ni nyumbani kwake. Alieleza hayo katika "From Great Zimbabwe to Kilimatinde" iliyochapishwa katika kitabu "More Great Railway Journeys."

Ni vibaya sana bado kuna Waafrika ambao wanaukana Uafrika wao.

Wakumbuke Waafrika walivyokuwa wanadharauliwa na Waarabu Zanzibar. Hata viongozi Waafrika walikuwa wanadharauliwa na viongozi wa Kiarabu. Kumbuka Juma Aley, waziri wa fedha na maendeleo katika serikali ya sultan, alivyomjibu Karume kwa dharau Karume alipomuuliza swali: hakuna haja na si lazima nijibu swali kutoka kwa mtu ambaye ni baharia tu. Katika hotuba nyingine Juma Aley alisema Waafrika ni wachache sana katika baraza la mawaziri kwa sababu hawana akili hata kidogo, Waarabu wamewazidi sana akili, hakuna sababu nyingine.

Na, mara tu baada ya uhuru, serikali ya sultan ilitangaza kwamba uhusiano wa Zanzibar na nchi zingine utakuwa kati ya Zanzibar na nchi za Kiarabu, hasa Egypt, bila kuwa na uhusiano wowote na nchi za Kiafrika za watu weusi. Waarabu waliiona Zanzibar kama nchi ya Waarabu, na ya Kiarabu, kama Egypt na nchi zingine za Kiarabu Afrika Kaskazini.

Upuuzi wote huo kutoka kwa viongozi wa Kiarabu katika nchi ambayo ni ya watu weusi, na ina watu weusi, Waafrika, kwa idadi kubwa sana kuliko watu wote wengine! Halafu kuna watu wanashangaa kwa nini mapinduzi yalitokea Zanzibar?

Inasikitisha sana bado kuna Waafrika ambao wanaona ni aibu kuwa Waafrika. Wanapenda Uarabu na kusema wao ni Waarabu. Wanapenda Uirani, Wanapenda Uzungu na kadhalika.

Kuna ambao wamekaa Merikani miaka miwili au mitatu, au minne, wakirudi Tanzania, wanasema wamesahau Kiswahili. Kuna ndugu yetu mmoja ambaye alirudi Tanzania baada ya kuishi Merikani zaidi ya miaka hamsini mfululizo na aliishi katka mji ambao hakuzungumza Kiswahili miaka yote hiyo kwa sababu hakukuwa na Watanzania na Wakenya miaka aliyoishi katika mji ule kuweza kuongea nao kwa Kiswahili. Mbona hakusahau Kiswahili? Hata matamshi yake ni kama yetu. Na anajua Kiingereza vizuri lakini hajisifu. Siyo mtu wa kujikweza, hana makuu, ni mtu wa kawaida sana, humble to a fault, na mkimya, ingawa amefanikiwa sana kwa maka mingi sana katika fani yake na anajulikana kakika nchi mbalimbali dunia nzima, si Tanzania tu.

Hao wengine wa miaka mitatu, minne, mitano na kadhalika, huko Merikani na vituko vyao wakirudi Tanzania, ukiwasikiliza, hawajui hata Kiingereza ingawa wanaseama ndiyo lugha hiyo tu wanayoijua baada ya kuondoka Tanzania na kusahau Kiswahili ghafla walipoingia Merikani. Wajaribu siku moja mkiwa nao ndani ya nyumba wawasikie mkisema, "Moto! Nyumba inaungua!" Ona watakavyoruka madirishani na kuvunja milango kuchomoka. Kiswahili kinarudi ghafla.


Ukiwasikiliza, Kiingereza chao kimejaa makosa, hata wanavyo andika hapa Jamiiforums. Kiingereza chao ni kuiga matamshi, na lafudhi, ya Black Americans, pamoja na slang. Sahau grammar, sahau standard English. Chao ni "You dig?" Badala "Do you understand?" "I'm hip," "I'm hip to that," "Hey, brotherman?" Many of them can't even spell well. Wanaandika "writte" badala ya "write" hapa hapa Jamiiforums hata baada ya kuishi Merikani zaidi ya miaka ishirini na tano.

Wengi wao wameishi Merikani zaidi ya miaka hiyo, zaidi ya miaka thelathini, hawajui hata tofauti kati ya "If I was" na "If I were," they don't even know what a subjunctive mood is, Kiingereza tulichofundishwa miaka yetu enzi ya Nyerere, hasa miaka ya sitini na mwanzoni mwa miaka ya sabini tulipokuwa secondary school. Wengi wetu, mimi nikiwa mmoja wao, tuliishia hapo bila kwenda chuoni. Lakini Kiingereza chetu ni cha afadhali, siyo kama cha ndugu zetu wanaorudi Tanzania na mbwembwe na kutema Ung'eng'e, Kimombo chao cha kubabaisha na kujifanya ni "black Americans" wamesahau Kiswahili. Unawasikia wanasema "I could care less" badala ya "I couldn't care less," "none sense" badala ya "nonsense" na kadhalika. Hata Trump aliwahi kusema "I could care less" zaidi ya mara moja. Walimsahihisha na kumwonya baada ya hapo. He is a moron. Sitaki kuamini ndugu zetu hao wako katika kundi hilo.

Ndiyo kasumba hiyo ambayo Waafrika wengi bado wanayo miaka mingi baada ya ukoloni. Ndiyo kasumba hiyo ya Wazanzibari wengi kusema wao ni Waarabu, ni Wairani, siyo Waafrika. Acheni kujipendekeza kwa watu who couldn't care less if all blacks were wiped off or vanished from the face of the earth.
Achana na kasumba. Jivunie uzalendo wako, Uafrika wako, badala ya kuwa laughingstock of the world.

Nakumbuka Nyerere aliyoandika katika kitabu chake "Freedom and Socialism": "Africans are not European and do not want to become European."

Kuna wengi wanaotaka kuwa hivyo na wanachukia walizaliwa Waafrika, watu weusi.

Hata baadhi yao, wanavyo oa, na wanavyo olewa, ni kwa sababu hiyo hiyo. Hata baada ya mapinduzi ilikuwa hivyo hivyo, kuwalazimisha wasichana wa Kiarabu kuolewa na wanaume wa Kiafrika wenye umri wa babu zao. Ilikuwa lulu, dhahabu, kwa hao wazee kujipatia wanawake wa Kiarabu! Walithibitisha uchu wao, tamaa waliyokuwa nayo miaka yote ya kuwapata wanawake wa Kiarabu kwa sababu "ni wazuri," "ni warembo," "ni bora" kuliko wanawake wa Kiafrika, wanawake weusi. Ni kasumba ilel ile! Na ni tusi kwa wanawake wa Kiafrika pamoja na dada zao, watoto wao wa kike, na hata mama waliowazaa wenyewe kwamba ni wabaya, siyo warembo, siyo wazuri kama wanawake wa Kiarabu as wa Kizungu.

Wanawacheka. Wanawadharau. Wanawatukana.

Hata katika ndoa, wako ambao wako hivyo, wanawake wanao watukana wanaume wa Kiafrika, wanaume weusi, kwa mfano Black Americans, ambao wametukanwa na wake wao au girfriends wao Wazungu, wakigombana, na kuambiwa, "You'e just a nigger to me," wengine, "You're nothing but a nigger," na kadhalika.

Hata Jerry Rawlings, raisi wa Ghana ambaye baba yake alikuwa ni mzungu, hakuwa na kasumba hiyo kudharalau na kuwa na aibu na Uafrika wake. Kuna wakati alisema: "I have a right to my identity, don't take away my identity. Christianize me if you may, but don't Europeanize me!"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…